Posts

HIVI TANZANIA TUNAKOELEKEA NI WAPI?KIONGOZI WA WANAFUNZI TANZANIA ABDUL NONDO NAYE ATOWEKA

Image
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo hajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka. Baba mdogo wa kiongozi huyo Mussa Mitumba akiwahutubia wanahabari pia ametoa wito kwa 'mwanawe' kurudishwa akiwa hai aendelee na kutafuta kutimiza ndoto zake. Abdul Nondo alituma ujumbe wa mwisho kusema alikuwa hatarini Kiongozi huyo wa wanafunzi alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo,Tahliso. Muungano huo unasema baada ya kuondoka afisi hizo,Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale. "Ghafla katika hali ya kutatanisha, kuanzia saa 6 hadi saa 8 usiku alijitoa kwenye makundi yote ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp jambo lililozua taharuki miongoni mwa watu wengi na kuanza kutaka kujua nin...

WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA HATARINI KUPATA KIPINDUPINDU

Image
Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Luhafwe kata ya Tongwe wilayani Tanganyika Mkoani Katavi  wamesema,wako  hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kuokana na maji wanayotumia kutokuwa safi na salama. Wakazi hao wameiambia Mpanda Radio kuwa,chanzo cha maji wanachokitegemea ambacho hakina maji safi na salama, kinaingiliwa na taka mbalimbali ambazo ndizo zinazosababisha wao kuumwa matatizo ya tumbo mara kwa mara. Aidha wamesema wanalazimika kutumia maji hayo kwa sababu hakuna chanzo kingine kinachoweza kuwapatia maji. Kwa mjibu mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw.Malaika Bujiku na katibu wake Paul Nkingwa Mabenga wamesema mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando alioneshwa chanzo hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali ili kuwanusuru wananchi na hali hiyo. Mapema mwaka 2016,serikali ya wilaya ya Tanganyika ilipitisha azimio la kujenga mji wa kibiashara katika eneo la Luhafwe lakini mpaka sasa huduma za kijamii kama shule,afya na maji bado zik...

MAJAMBAZI WAUA,WAJERUHI NA KUPORA MALI MGODINI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwa rasasi   sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi   usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi. Pamoja na kuwataja majeruhi,kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya(21) mkazi wa kata ya machimboni Wilayani Mpanda aliyepigwa risasi mgongoni na kutokezea tumboni.

MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS

Image
  Jacob Gedleyihlekisa Zuma   alizaliwa  Aprili 12, 1942 . Ni Rais wa  Afrika Kusini  tangu 2009.Alikuwa makamu wa rais chini ya  Thabo Mbeki  kati ya 1999 na 2005.Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha  ANC . KIJANA NA MWANAHARAKATI WA ANC Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la  Kwa Zulu-Natal .Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya  apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko  Robben Island  pamoja na  Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko  Msumbiji  na  Zambia na aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC. KUPANDA NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha ...

HATIMAYE RAIS ZUMA AJIUZULU

Image
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamua kujiuzulu mara moja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa chama chake kinachotawala nchini humo cha African National Congress, ANC. Chama tawala nchini Africa kusini cha ANC,kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais. Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ameongeza kwa kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo,kutokana na kuwa Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60. Awali kupitia televisheni Bw.Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake. Makamu wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo. Zuma alikilalamikia chama cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani,ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya...

BARAZA LA MADIWANI LACHARUKA UPIGAJI CHAPA MIFUGO CHINI YA KIWANGO

Image
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limewajia juu wataalamu wake kwa kutotekeleza kwa weledi upigaji chapa mifugo na kuwatishia kuwa watalamika kwenda kurudia zoezi hilo kwa gharama zao iwapo alama zinazowekwa zitafutika baada ya muda mfupi.   Katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kilichofanyika Mjini Kiomboi, ajenda iliyochukua uzito mkubwa ni juu ya kufutika kwa alama zilizowekwa kwenye upigaji chapa mifugo na kuchelewa kwa malipo ya wananchi walioshiriki  kusaidia  utekelezaji wa zoezi hilo.  Afisa mifugo Wilaya ya Iramba Andrew Manyerere anasema kuwa ingawa zoezi hilo lilitekelezwa kwa kuzingatia sheria lakini kwa mifugo ambayo alama zake zimefutika watarudia  bila malipo. Hata hivyo uamuzi wa baraza la madiwani wa uliotolewa na Mwenyekiti wake Simion Tyosela ni kwa wataalamu kufanyakazi hiyo kwa weledi vinginevyo watarudia zoezi hilo kwa gharama zao. Zaidi ya shilingi milioni 16 zi...

RAIS JACOB ZUMA ASEMA HAONI SABABU YOYOTE YA KUJIUZULU

Image
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu. Bw.Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu vinginevyo atakabiliwa na kura isiokuwa na imani dhidi yake leo Alhamisi. Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu Rais huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya ufisadi lakini amesema ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu. Bw.Zuma amesema yuko tayari kuondoka baada ya mwezi Juni lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa na alisema atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano. Chama cha ANC kimesema kilisikiza matamshi ya Bw.Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua yake baadaye kabla ya kuzungumza. Kiongozi wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kuwa kura isiokuwa na imani dhidi ya rais itasikilizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba akiap...