Posts

KIM JONG-UN AMUALIKA RAIS WA KOREA KUSINI

Image
Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kuzuru Pyongyang ambapo Utakuwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi hao wa Korea. Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini Bw.Moon amesema Korea ni muhimu kuhakikisha mkutano huo unafanyika huku akiitaka Korea Ksakzini kurudi katika meza ya mazungumzo na Marekani. Mualiko huo ulioandikwa ulikabidhiwa kwa rais wa Korea Kusini na dadake rais Kim Jong un,Kim Yo Jong ambapo Katika mkutano wa kihistoria uliofanyika katika jumba la rais kabla ya kuanza kwa michezo hiyo ya msimu wa baridi. Bi.Kim na kiongozi wa kisherehe wa taifa la Korea Kaskazini Kim Yong-nam ndio viongozi wa ngazi za juu kutoka Kaskazini kuzuru kusini tangu vita vya Korea 1950. Rais Donald Trump na mwenzake wa Korea Kusini Kim Jae-in Wakati huohuo Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae amekuwa ni mwenye shughuli nyingi za kupokea ujumbe wa ngazi ya juu katika ikulu yake ya mjini Seoul...

MH.SUGU NA MASONGA WAACHIWA KWA DHAMANA HUKUMU YAO FEBRUARI 26,2018

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi''SUGU'' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA MABALOZI NA WAKUU WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Joseph Magufuli amewahakikishia mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika kipindi cha mwaka 2018 serikali ya awamu ya tano itaendeleza juhudi za kuendeleza mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa,kuboresha miundombinu ya barabara,reli na usafiri wa anga,kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika mwaka 2018 Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuboresha miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga, kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya biashara. Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 09 Februari, 2018 katika hafla ya mwaka mpya aliyowaandalia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao ...

WAZIRI AAGIZA WALIONYANG’ANYWA PIKIPIKI NA POLISI KURUDISHIWA

Image
WAZIRI wa Mambo ya Ndani,Dkt.Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo. Dkt.Nchema amesema waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu. Dkt.Mwigulu amesema zile zenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita,madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza huku akisema zenye makosa madogo wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

MAGAIDI WAWILI HATARI WA IS WAKAMATWA

Image
Raia wawili wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd. Alexanda Kotey(34) na mwenzake El Shafee Elsheikh(29) ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kukamatwa. Image caption Magaidi Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh Kundi hili la vijana wanne kutoka raia wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa ni kundi hatari linalofahamika kama Beatles hiyo ikiwa ni kutokana na lafudhi yao wanapozungumza.

CHADEMA WAZUNGUMZIA KIFO CHA KADA WAKE MKONGWE

Image
Mwenekiti wa Chadema taifa Mh.Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza. Amesema kuwa Hizza alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM. Mbowe amesema hayo jana Februari 8 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana. Kufuatia kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia matamanio ambayo kiongozi huyo alikuwa akiyatamani.

TANZANIA KUWA NA WATU 58 MILIONI IFIKAPO MWISHONI MWA 2018

Image
Tanzania inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni 58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na idadi ya awali ya watu milioni 46 iliyoripotiwa mwaka 2010. Kwa mujibu wa Idara ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN),makadirio hayo ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67 tofauti na makadirio ya mwaka 2010 ya watu 52. Inasema kila sekunde 14,mtoto mmoja anazaliwa nchini huku mtoto mmoja akifariki dunia kila baada ya sekunde moja.