Posts

SIKU 11 ZA VIKAO VYA BUNGE KUANZA KESHO JANUARI 30,2018

Image
Bunge la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza mkutano wa 10 wa Bunge hilo kuanzia kesho Januari 30. Kwa mjibu wa taarifa ya bunge ambayo imetolewa leo na kitengo cha habari,elimu na mawasiliano kutoka Ofisi ya Bunge inaeleza kuwa miongoni mwa shghuli za kesho ni pamoja na kiapo cha uaminifu kwa wabunge wateule watatu ambao ni Mh.Dkt.Damas Daniel Ndumbaro mbunge wa Songea Mjini,Mh.Monko Justine Joseph mbunge wa Singida Kaskazini na Mh.Dkt.Stephano Lemomo Kiruswa. Aidha kwa mjibu wa taarifa hiyo kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu,miswada ya serikali pamoja na taarifa za kamati za kudumu za bunge. Vikao hivyo vinavyoatarajia kuanza kesho vinatarajia kufikia tamati Februari 9 mwaka huu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

NECTA YATANGAZA TAREHE YA MTIHANI KIDATO CHA SITA

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu kidato cha sita inatarajia kuanzaitaanza Mei 7 hadi 24 mwaka huu. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Necta Januari 26, mwaka huu,inaonyesha somo la kwanza litakuwa ni masomo ya jumla ‘General Studies’ na somo la mwisho litakalofanyika Mei 24 litakuwa ni Baiolojia 3C (kwa vitendo). Msemaji wa Necta,John Nchimbi amesema “lengo la kutoa ratiba ni kuwafanya wanafunzi na walimu wao kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao.” Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

DK.SLAA AKUTANA NA RAIS IKULU JIJINI DAR,MAAFISA WASTAAFU WA JWTZ NAO WAAGANA NA RAIS

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Mhe.Dkt. Wilbrod Peter Slaa Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya Mazungumzo hayo Balozi Mteule Mhe.Dkt. Slaa amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Balozi na ameahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Mhe.Dkt.Slaa amempongeza Mhe.Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora wenye maono na uthubutu wa kutekeleza mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ( Standard Gauge ),ujenzi wa daraja la juu ( Flyover ) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela ( Tazara ),mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ( Stieglers’ Gorge ) na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Dkt. Slaa kwa moyo wake wa kizalendo na amesema aliamua kumteua ...

WAZIRI APIGA MARUFUKU MADARASA YA NYASI,TEMBE,UDONGO KATIKA SHULE ZOTE NCHINI

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora. Waziri wa Tamisemi Mh.Suleiman Jafo Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi. Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi  kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini. Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya kuheshimu  mipaka yao ya kazi,mahusiano kazini,kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo y...

HABARI PICHA MKOANI KATAVI WAKATI WA UFUNGUZI WA WIKI YA SHERIA

Image
Askari katika maandamano ya ufunguzi wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Katavi katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Muhando na Mkuu wa Wilaya Mpanda Lilian Charles Matinga wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Watumishi wa mahakama wakishikilia bango wakiwa sambamba na wanafunzi katika Manispaa ya Mpanda wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Wanafunzi wa shule mkoani Katavi wakishiriki maandamano katika uzinduzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Watumishi wa mahakanma katika maandamano ya uzinduzi wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi (PICHA NA.Issack Gerald) Bango wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria Tanzania Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MAHAKAMA KUPATA HAKI

Image
Wananchi Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga tabia ya kuitumia mahakama kama Chombo cha kupatia haki kama kichocheo cha kuimarisha dhana ya Utawala bora  hapa Nchini. Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Muhando wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria  ambayo imeanza kuadhimishwa katika Viwanja vya mahakama ya  wilaya Mpanda. Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama mkoani Katavi,MH Ommary Hassani Kingwele amesema dhima kubwa ya uwepo wa wiki ya elimu ya sheria ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata uelewa wa sheria. Madhimisho hayo ya sheria mwaka huu yaliyo na kauli mbiu ‘’ matumizi ya tehama katika utoaji haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili ’’ kilele chake kitakuwa Februari moja mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi meja jenerali mstaafu Rafael Muhuga. H...

MAHAKAMA YA RUFAA YAWAKANA CHADEMA

Image
Mahakama ya Rufaa imesema hakuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido iliyopo mahakamani hapo. Mahakama hiyo imetoa kauli hiyo wakati Chadema ikiilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo kwa madai kwamba kuna kesi mahakamani hapo. Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema Onesmo ole Nangole ushindi wake kutenguliwa na Mahakama Kuu. Mara kadhaa Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe na Ole Nangole wamekaririwa na vyombo vya habari wakidai kuna rufaa katika Mahakama ya Rufani. Viongozi hao wamekuwa wakiilalamikia NEC kuwa iliendesha uchaguzi mdogo katika jimbo hilo wakati rufaa ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomvua ubunge Ole Nangole ikiwa haijatolewa uamuzi. Hata hivyo,Mahakama ya Rufaa imesema uchaguzi mdogo uliofanyika Longido ulikuwa halali kwa kuwa hakuna rufaa yoyote iliyoko mahakamani hapo. Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa,Elizabeth Mkwizu amesema hakuna ruf...