Posts

WAZIRI AVUNJA BODI

Image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe hii leo amevunja Bodi za Wakurugenzi za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Jiji la Arusha na Musoma. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiy Prof.Kitila Mkumbo imeonesha Waziri Kamwelwe amesema kuwa amefanya hivyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bodi hizo. Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa tayari mchakato wa kuunda bodi mpya umeanza na zitatangazwa mara zitakapokamilika. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WABUNGE 11 WAVULIWA UANACHAMA

Image
Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe jana kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe. Maamuzi ya kuvuliwa uanachama wabunge hao yalitolewa na kutangazwa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge la Zimbabwe,Mabel Chinomona baada ya Bunge hilo kupokea barau kutoka kwenye chama cha ZANU PF iliyosema wabunge hao wamefukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe kupitia kifungu namba 129 (1) (k). Naibu Spika alisema kuwa wabunge waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, aliyekuwa Waziri wa Nishati,aliyekuwa Waziri wa Michezo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na wabunge wengine wa majimbo mbalimbali nchini humo.  Kufuatia zoezi hilo Bunge limetangaza nafasi wazi katika majimbo hayo 11 na kuijulisha Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuhusu uwepo wa nafasi za wazi katika majimbo hayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kupata wawakilishi wa Wanachi.  Habari zaidi ni P5T...

MSIMAMO MPYA WA RAIS MSEVENI KUHUSU KUNYONGA WATU

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anatafakari uwezekano wa kuanza tena kuwanyonga wahalifu nchini humo. Rais Museveni amesema licha ya kwamba yeye ni "Mkristo" kuwa dini yake imemzuia kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wale ambao wamehukumiwa kunyongwa, hata hivyo amesema hali hiyo imekuwa ikiwatia moyo wahalifu. Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kuhitimu kwa askari wa idara ya magereza katika gereza la Luzira jijini Kampala. Mpaka sasa ni miaka 13 sasa tangu Uganda ilipotekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu. Watetezi wa haki za kibinadamu wameshutumu tamko hilo la Rais Museveni na kusema adhabu ya kifo haikomeshi uhalifu. Mara ya mwisho kwa Rais Museveni kuidhinisha hukumu ya kifo itekelezwe ilikuwa katika gereza la Luzira mwaka 1999 na mwaka 2005 aliidhinisha mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya kifo Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI WILAYANI MPANDA WALALAMIKIA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA RELI

Image
Wananchi wilayani Mpanda   mkoani Katavi wamelalamikia shirika la reli kwa kutorekebisha miundombinu ya reli kwa wakati   katika eneo la Ugala mpaka Rumbe. Wananchi hao wameeleza kuwa kumekua na ajali nyingi zikitokea kutokana na miundombinu ya eneo hilo kutokuwa salama kwa usafiri hali inayosababisha kupotea kwa mizigo. Mkuu wa kituo cha reli  Mpanda  Bw.Vivian Lyapembile amesema kuwa pamoja na changamoto wanazopata  kwa sasa  ila wana ufahamu na  tatizo hilo na tayari wameanza mchakato wa kukarabati eneo hilo. Hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya usafiri kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa treni hali inayosababishwa uchakavu wa miundo mbinu kwa baadhi ya maeneo pamoja na maeneo mengine reli kusombwa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.  Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOANI WA RUKWA WAZINDUA KAMPENI YA UPANDANI MITI

Image
MKOA wa  Rukwa umezindua kampeni ya upandaji miche ya miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira ambapo katika kipindi cha mwaka huu unatarajia kupanda jumla ya  miche milioni sita katika halmashauri zote nne za mkoa huo. Akizundua kampeni katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai,mkuu wa mkoa huo Joachim Wamgabo alisema kila halmashauri italazimika kupanda miche isiyopungua milioni 1.5 ambapo mpaka sasa tayari mkoa mzima umeotesha miche milioni 2,173,649 sawa na asilimia 36 ya miche itakayo pandwa. Alisema yeye  amezindua kampeni hiyo kinachofuata ni watendaji wa serikali kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza na ambapo itakapofikia mwishoni mwa mwaka halmashauri ambayo haitafikia lengo itatozwa faini ya shilingi milioni moja na fedha hizo itakabidhiwa halmashauri ambayo imetekeleza kampeni hiyo kwa asilimia mia moja. Awali kabla ya kuzindua kampeni hiyo Wangabo alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Simon Ngagani amw...

WATOTO 400 WAKOSA ELIMU WILAYANI SUMBAWANGA

Image
JUMLA ya watoto wa wavuvi wapatao 400 waliopo katika kambi ya wavuvi ya Nankanga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ambao wamefikia umri wa kuanza darasa la kwanza wameshindwa kupata haki yao ya elimu kutokana na kutokuwa shule. Diwani wa kata ya Nankanga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, Anyisile Kayuni alimwambia hayo mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo wakati akiwa katika ziara ya kukagua makambi ya wavuvi katika suala la kukabiliana na ugonjwa wa kipindu pindu. Alisema kuwa watoto hao wanaishi na wazazi wao katika kambi hiyo ya Nankanga iliyopo katika kijiji cha Nankanga,kata ya Nankanga na wamefikia umri wa kuanza shule ya msingi lakini wameshindwa kutokana na kuwa katika eneo walilopo hakuna shule. Diwani huyo alisema kuwa shule ya msingi ipo umbali wa kilomita tisa kutoka yalipo makambi hayo umbali ambao ni mkubwa huku ukikabiliwa na changamoto ya barabara kitendo kinachosababisha washindwe kwenda shule. alisema kuwa kwa kuliona hilo yeye kupitia uongizi wa makambi hayo wal...

WILAYA YA NKASI YATANGAZA VITA DHIDI YA WANAUME WANAORUBUNI WANAFUNZI KUSHIRIKI MAPENZI.

Image
KATIKA kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi wanaume wilayani Nkasi  Mkoani Rukwa wameonywa  kuacha mara moja tabia ya kuwaita watoto hao wa kike majina ya mahaba kwani yanawapelekea kujiona wamekua na kuanza kushiriki vitendo vya ngono. Wito huo umetolewa jana na afisa elimu Sekondari wilayani Nkasi Abel Ntupwa  kwenye kikao kazi kilichowajumuisha Wakuu wa shule 23 za sekondari wilayani Nkasi  kilichomshirikisha na afisa elimu wa mkoa Nestory Mloka kilicholenga kupeana mikakati namna ya kuboresha taaluma baada ya wilaya Nkasi kuporomoka sana kwenye mitihani ya kitaifa. Alisema hivi sasa watu wazima wamekua na tabia ya kuwaita watoto hao wa kike ambao ni Wanafunzi majina ya kimahaba kama  Baby kama mzaha na mwisho wa siku ujikuta Watoto hao wanajiingiza kwenye mtego huo mbaya na hivyo kuanza kushiriki vitendo vya mapenzi. Hivyo  kufuatia hari hiyo amedai kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote  kumwita mtoto wa kike ambaye ni...