Posts

MASHEHE 5 MKOANI KATAVI WAMEJIUZURU

Image
Na.Issack Gerald Mashehe watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari wamesema kujizulu kwao ni kutokana na shehe wa Mkoa wa Katavi kukiuka Katiba ya Bakwata. Katika picha ni Shehe Mashaka Kakulukulu miongoni mwa waliojiuzuru Wajumbe waliojiuzulu wakiwemo Mashehe Mohamad Shaaban Sigulu na Said Haruna Omary wamemtuhumu Shehe wa Mkoa Ally Hussein kuwa kinara wa kukiuka kat iba ya Bakwata. Wajumbe wengine wa baraza la mashehe Mkoa waliojiuzuru ujumbe ni Shehe Mashaka Nassoro Kakulukulu na Hassan Mbaruku. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoani Katavi Shehe Shaban Bakari ambaye naye juzi amejiuzuru,amesema Shehe wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein amekuwa akizuia maendeleo ya dini ya kiislamu kwa kutokubaliana na maamuzi ya vikao halali huku akiunga mkono waharifu na wanaopinga maendeleo ndani ya dini. Aidha Shehe Bakari amesema sababu nyingine ambayo imewafanya wajiuzuru ni baada ya shehe...

TAAS MKOANI KATAVI WAMEKATAA KUITWA WALEMAVU WA NGOZI

Image
Na.Issack Gerald Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye ulemavu wa ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino. Mwenyekiti wa TAAS Mkoani Katavi Victus Kweka Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za w atu wenye ulemavu kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu,afya na haki nyingine za kibinadamu. Amesema rangi ya ngozi waliyonayo watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao wanahesabika katika kundi la watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali waliyonayo. Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa. Amewataka watu wenye ualbino kuchanganyikana na jamii ili kupata elimu inayowawezesha kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya kupu...

WAZIRI WA MAJI NAYE AMTUMBUA MHANDISI WA MAJI MKOANI RUKWA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amemsimamisha kazi Mhandisi Goyagoya Mbena kwa tuhuma za kusaini barua ya kuruhusu ujenzi wa mradi wa Maji wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Taarifa ambayo imetolewa jana na Wizara hiyo,imeeleza kuwa Mhandisi Mbena amesaini barua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo kinyume cha utaratibu. Mradi huo wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa u meelezwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7.4. Siku ya Juzi Waziri wan chi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mh.Suleiman Jafo,alimsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Julius Kawondo kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni. Chanzo:eatv Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MVUA YA LEO MKOANI KATAVI IMELETA MADHARA

Na.Issack Gerald Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Katavi zimesababisha madhara katika makazi ya wakazi wa Mtaa wa Misunkumilo uliopo Manispaa ya Mpanda ukiwemo uharibifu wa miundombinu. Baadhi ya wananchi ambao makazi yao yameharibiwa ikiwemo kufa kwa mifugo kutokana na maji kukosa mwelekeo hali inayosababishwa na kutokuwepo kwa mitaro ya maji wameiomba serikali ichukue hatua. Kwa upande wa Mwenyekiti wa mtaa huo BW Katabi Jona ameutaka uongozi wa Manispaa kuichukulia hatua Kandarasi iliyo husika na ujenzi wa barabara za mtaa huo bila kuweka mitaro. Haya yana jili ikiwa ni siku moja tu tangu mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA kutoa tahadhari juu ya uwepo wa Mvua kubwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI JAFO AMTUMBUA MKURUGENZI MKOANI RUKWA

Na.Issack Gerald Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Bw.Julius Kaondo. Waziri Jafo katika kikao na Waandishi wa habari,amesema amemsimamisha Bw.Kaondo kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kushindwa kusimamia mradi wa maji. Kufuatia hatua hiyo,Waziri Jafo ametoa agizo k wa wakurugenzi watendaji na watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa na amewataka wasimamie wajibu wao kama inavyotakiwa katika kutekeleza majukumu anayotakiwa kuyatekeleza kwa mjibu wa miongozo ya nchi. Jafo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia vifungu vya sheria za nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwezi uliopita Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba walifukuzwa kazi na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kushindwa kujibu maswali yake akitaka kujua kiwango cha fed...

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO WANAKABILIWA NA KITISHO CHA HAKI ZAO KUTOPATIWA KIPAUMBELE

Na.Issack Gerald Imebainika watu wenye ulemavu Mkoani Katavi bado wanakabiliwa na kitisho cha haki zao za msingi kutopati wa kipaumbele na hivyo kuchochea unyanyapaa kuendelea kuwa mkubwa dhidi ya makundi hayo. Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa kupinga ukatiri dhidi ya watu wenye ulemavu na kujadili namna matatizo ya watu wenye ulemavu yanashghulikiwa. Kwa upande wa mratibu wa mradi wa elimu jumuishi Mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza pamoja na mratibu wa mradi huo Mkoani Katavi Raphael Fortunatus,wameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakumba watu wenye ulemavu katika Mkoa ya Rukwa na Katavi. Mkurugenzi wa Shirika la International Aid Service(IAS) kutoka nchini Denmark Bw.Torben Madsen mara baada ya kikao cha leo,amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu hasa katika sekta ya elimu. Makundi ya Mtandao wa wazazi wenye ulem...

RAIS MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157 IMO FAMILIA YA BABU SEYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wanaotakiwa kutolewa siku ya leo wakiwa ni 1,828. Papii Kocha na Nguza Viking Rais ametoa msamaha huo leo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika Mjini Dodoma Leo. Rais Magufuli amesema amezingatia ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompatia rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa . Miongoni mwa waliotangaziwa kusamehewa ni pamoja na Nguza Viking anayefahamika pia kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha waachiwe huru kuanzia leo. Wakati huo huo wafungwa 61 waliotakiwa kunyongwa hadi kufa wamesamehewa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED