Posts

LEO NI SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

Na.Issack Gerald Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imethibitisha kuwa leo kutakuwa na Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu Duniani. Kauli hiyo imethibitishwa na Idara za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii za Manispaa hiyo na kuwataka wananchi kujitokeza na kushiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili. Miongoni mwa maafisa ambao wamethibitisha kuwepo kwa maadhimis ho hayo ni pamoja na afisa maendeleo ya jamii Bi.Marietha Mlozi kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mpanda. Katika Mkoa wa Katavi inakadiriwa kuwa kuna watu wenye ulemavu wapatao zaidi ya 2000 ambao wamegawanyika katika makundi ya wasioona,viungo,ualibino,viziwi na wenye mtindio wa ubongo(Masonji). Sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la Tanzania mwaka 2010 inaitaka serikali na jamii kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu yanapatiwa haki sawa na watu wasio na ulemavu katika haki za kibinadamu. Kitaifa maadhimisho...

MBUNGE NASSARI:NIMENUSURIKA KUUWAWA KWA RISASI USIKU

Image
Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake. Mh.Joshua Nassari Katika ukurasa wake wa twitter,Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao wamevamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo wamewafyatulia mbwa wake. Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kuwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara. Hakuna kauli ya jeshi la polisi ambayo imetolewa kuzungumzia tukio hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMEKANUSHA UWEPO WA PEMBEJEO FEKI

Image
Na.Issack Gerald Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imekanusha kuhusu uwepo wa pembejeo feki zinazosambazwa na kutumika katika msimu huu wa kilimo. Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa halimashauri hiyo Bw. Fabian Kashindye ambapo ameeleza kuwa kitisho hicho ni sawa na propaganda. Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania hutegemea kilimo katika kuendesha maisha na kipato cha kaya,wengi wao ni kutoka vijijini ambao hukabiliwa na elimu duni kuhusu kilimo bora. Hivi karibuni Waziri wa Kilimo,Dk Charles Tizeba ameitaja mikoa ya Rukwa,Njombe,Iringa,Songwe na Mbeya kuongoza kwa kuuza mbegu feki za mahindi na kusababisha madhara makubwa kwa wakulima, ikiwemo uzalishaji mdogo wa zao hilo Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WAMELALAMIKA KUNYANG’ANYWA GARI LA WAGONJWA,HALMASHAURI YATOA UFAFANUZI

Image
Na.Issack Gerald Wakazi wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa madai kuwa halmashauri hiyo imewanyanga’anya gari la wagonjwa ambalo limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa katika kata hiyo. Wamesema kuwa wamenyang’anywa gari kwa madai kuwa wakazi wa Katumba hawana dereva wa kuendesha gari hilo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mh.Raphael Kalinga amekanusaha kuwanyang’anya gari la wagonjwa wakazi wa Kata ya Katumba ambapo amesema lipo kwenye matengenezo baada ya kuharibika. Aidha Kalinga amesema suala la kuharibika kwa gari hilo limekwishatolewa ufafanuzi kuanzia kwa viongozi wa Halmashauri,Mkoa hadi ngazi ya wizara. Kata ya Katumba ina vijiji 16 na zaidi ya wakazi elfu hamsini wanaotegemea huduma ya gari hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MAADHIMISHO YA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO KIZUNGUMKUTI

Na.Issack Gerald Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi (SHIVYAWATA)limesema mpaka sasa hawana uhakika wa kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani kwa sababu ya uhaba wa pesa. Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw.Issack Mlela wakati akizungumzia maandaliza ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu inayaotarajiwa kuadhimishwa Desemba 3 mwaka huu. Kwa   upande wake Katibu wa chama cha watu wenye ulemavu mkoani Katavi Bw.Godfrey Sadara pamoja na kuitaka jamii kuwafichua watu wenye ulemavu waliofichwa majumbani pia amesema unyanyapaa unaoendelea dhidi ya kundi hilo linatakiwa kukemewa na kila mmoja. Asasi ya kiraia ya IFI inayohusika na masuala ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi kupitia kwa mratibu wake Raphael Fortunatus imesema bado serikali ni kama imesahau makundi ya watu wenye ulemavu katika kuwawezesha ili wafanye maadhimisho. Zaidi ya shilingi milioni moja inatakiwa ili kufanikisha maadhimisho ya watu we...

WAKAZI KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO HAWANA MAJI KWA ZAIDI YA MIEZI 6

Na.Issack Gerald WAKAZI wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia serikali kwa kutoshughulikia tatizo la maji kata ya katumba ambapo kwa sasa hawana maji kwa muda wa miezi 6. Wakazi hao wametoa malalamiko hayo kwa Nyakati tofauti wakati wakati wakizungumza kuhusu tatizo la maji linalowasumbua kwa sasa ambapo wamesema limesababishwa na mashine iliyokuwa   ikisukuma maji kuharibika. Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji Bw.Ngeze Joel amekiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema tatizo la maji limetokana na kuharibika kwa mashine huku Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B Kombo Masatu amesema baadhi ya vifaa vimenunuliwa ili kumaliza tatizo. Mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni Hussein Nasri mahali Mashine hiyo ilipo kwa upande wake amesema hakuna mwelekeo wa lini ufumbuzi utapatikana. Kwa mjibu wa Bw.Hussein Nasri Mashine hiyo yenye thamani ya karibu shilingi milioni 80 inasamabaza maeneo ya huduma za jamii kama soko,shule,kituo ...

WANANCHI MKOANI KATAVI WAMEZUNGUMZIA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Image
Na.Issack Gerald Baadhi ya wananchi mkoani katavi wamesema ni vyema jamii kubadili tabia ikiwemo kuachana na ngono zembe ili kuweza kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi. Mapema leo hii wamebainisha hali hiyo wakati wakizungumzia namna wanavyoielewa siku ya ukimwi duniani ambapo wananchi hao akiwemo Mwajuma Idd Bakary na Islam Said wamesema elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi wamekuwa wakiipata na wameweza k uwahamasisha wengine kupima afya zao. Sanjari na hayo pia  wamewaasa vijana kuhakikisha wanapima afya zao mara kwa mara na kuwa mabalozi kwa wengine namna ya kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi. Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa Ukimwi ambapo kwa miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Katavi una asilimia 5.9. Siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 ya kila mwaka na kauli mbiu kwa mwaka huu inasema  “Changia mfuko wa maisha,Tanzania bila Ukimwi inawezekana” Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED