LEO NI SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI
Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi imethibitisha kuwa leo kutakuwa na Maadhimisho ya siku ya watu
wenye Ulemavu Duniani.
Kauli hiyo imethibitishwa na Idara za
Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii za Manispaa hiyo na kuwataka wananchi
kujitokeza na kushiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Kashaulili.
Miongoni mwa maafisa ambao
wamethibitisha kuwepo kwa maadhimisho hayo ni
pamoja na afisa maendeleo ya jamii Bi.Marietha Mlozi kutoka idara ya Maendeleo
ya Jamii Manispaa ya Mpanda.
Katika
Mkoa wa Katavi inakadiriwa kuwa kuna watu wenye ulemavu wapatao zaidi ya 2000
ambao wamegawanyika katika makundi ya wasioona,viungo,ualibino,viziwi na wenye
mtindio wa ubongo(Masonji).
Sheria
namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la Tanzania mwaka 2010 inaitaka
serikali na jamii kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu yanapatiwa haki
sawa na watu wasio na ulemavu katika haki za kibinadamu.
Kitaifa
maadhimisho haya yanayoadhimishwa Desemba 3 ya kila mwaka yataadhimishwa Mkoani
Simiyu na kauli mbiyu ya mwaka 2017 inasema‘’Badilika
tunapoelekea jamii Jumuishi na imara kwa watu wote’’.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments