Posts

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU AMEMJULIA HALI MH.TUNDU LISSU

Image
Na.Issack Gerald Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Mhe.Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake. Mhe.Tundu Lissu amemshukuru Mhe.Rais Magufuli na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao. Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED

RAIS KENYATTA AMEANZA SAFARI YA PILI MUHULA WA PILI WA URAIS

Image
Na.Issack Gerald Hatimaye jana Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kwa muhula wa pili wa miaka mitano katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Kasarani mwezi mmoja baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi uliosusiwa na mpinzani mkuu Raila Odinga. Kulikuwa na nderemo na shangwe katika uwanja huo kutoka kwa maelfu ya wananchi wengi wao wafuasi wa muungano wa chama tawala cha Jubilee waliojaa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani. Uwanja huo unaingiza watu 60,000 lakini habari zinasema walioingia walikuwa 100,000. Wageni waalikwa na watu mashuhuri wapatao 40 walihudhuria sherehe hizo wakiwemo zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 10. Kenyatta,55,alishinda uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26 kwa asilimia 98.Uchaguzi huo ulifanyika baada ya matokeo ya ushindi wa Agosti 8 kufutwa na Mahakama ya Juu kwa maombi ya Odinga aliyewasilisha ushahidi wa dosari na ukiukwaji wa katiba. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  ni miongoni viongo...

KASI YA KUMNASUA MTOTO WA KIKE HASA MIMBA ZA UTOTONI YAZIDI KUSHIKA KASI

Na.Issack Gerald WATOTO wa kike mkoani Rukwa wamepewa mafunzo maalumu ya namna ya kuzitambua changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kuzitumia fursa zilizopo katika kutekeleza matarajio yao ili waweze kujitegemea. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi uitwao U-report unaotekelezwa na Tanzania Girl Guides Association mkufunzi wa mradi huo,Emiliana Stanslaus amesema wahitimu wapatao 20 katika kila halmashauri wamewezeshwa namna ya kuwasaidia wasichana wenzao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi yao. Amesema wasichana hao walipata mafunzo ya siku mbili ambapo watawasaidia wanafunzi wenzao wa kike katika shule za msingi na sekondari na wasichana waliopo vijijini katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kubakwa na pia kupata mimba za utotoni. Emiliana amesema mradi huo utatekelezwa katika halmashauri za Sumbawanga vijijini,Kalambo,Nkasi na Sumbawanga Manispaa kwa njia ya kutuma ujumbe wa maandishi ya simu kwenda namba maalumu ya 150...

RAIS MAGUFULI ASISITIZA JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA

Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwa sababu yeye ndiye rais kwa sasa tofauti na zamani alipokuwa waziri. Rais amesema hayo mapema leo wakati akihutubia wananchi ambao wamejitokeza katika ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila. Aidha rais Magufuli amesema Jengo hilo lazima libomolewe hata nusu ya jengo iliyopoo katika hifadhi ya barabara huku akisema na kama ni kuondoa jengo lote basi inamaanisha kuwa pia jengo la wizara ya maji nalo itabidhi liondolewe kwa kuwa sheria ni msumeno. Wakati huo huo rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwa sababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara na waliotakiwa kulipiwa fidia walikwishalipwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOA WA KATAVI UMEZINDUA SIKU 16 ZA KUPAMBA NA AKATIRI WA KIJINSIA

Na.Issack Gerald Mkoa wa Katavi umezindua siku 16 za kupinga ukatiri wa Kijnsia uzinduzi ambao umefanyika katika kata ya Kabungu wilayani Tanganyika ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 12 mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi huo,kamanda wa Polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amesema makosa ya ubakaji yamepungua kutoka matukio 100 kwa mwaka na kufikia matukio 68 kwa mwaka huu ambayo yameripotiwa. Aidha Kamanda Nyanda amewapongeza wananchi kwa kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutoa taarifa mbalimbali ikiwepo za ukatili unaoendelea kutokea sehemu mbalimbali za mkoa huu. Kwa upande wao wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Katavi katika risala yao wameomba mkoa kutafuta njia za kupunguza au kumaliza tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa ni miongoni mwa sababu inayosababisha vifo kwa watoto wengi kutokana na uzazi. Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi Meja jenerali Rafaeli Muhuga mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wananchi kuacha kufuata mila potofu zi...

RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Mh.Uhuru Kenyatta. Taarifa ya serikali ambayo imetolewa na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi imethibitisha hilo. Mhe.Kenyatta anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Nairobi ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo. Rais Uhuru Kenyatta atakuwa anaongoza Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTOIOGOPA MAHAKAMA

Na.Issack Gerald Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoiogopa mahakama kwa kuwa ipo kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wananchi katika kupatikana na kwa haki zao. Wito huo umetolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Mh.David Daniel Mbembela kupitia kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa cha Mpanda Radio. Aidha amewashauri wananchi kujenga tabia ya kufika katika mahakama kwa ajili ya kujifunza namna kesi zinavyoendeshwa mahakamani. Wakati huo huo Mh.Mbembela amesema serikali imeleta baraza la ardhi la wilaya mkoani Katavi kwa ajili ya kusikiliza migogoro na kesi zinazohusu masuala ya ardhi ambapo awali wakazi wa Mkoa wa Katavi walikuwa wakipata huduma hiyo wilayani Sumbawanga Rukwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED