WANAHARAKATI WAMETAKA SHERIA ZINAZOHUSU WATU WENYE ULEMAVU ZIWE HAI
Na.Issack Gerald-Mpanda Wanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kusimamia kanuni na sheria za nchi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu kama zilivyoainishwa katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Wanaharakati hao wakiwemo mtandao wa wazazi,Shivyawata, wajumbe wa baraza la watoto wilayani Mpanda na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu,wametoa kauli hiyo leo katika kikao cha kujadili haki za watoto wenye ulemavu kikao ambacho kimefanyika mjini Mpanda. Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael Fortunatus Jumbe pamoja na mambo mengine amesema semina ya leo inalenga kufikisha elimu kwa wanaharakati ili washiriki kupaza sauti katika kutetea haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuwafichua watoto waluiofichwa majumbani. Kwa mjibu wa vifungu vya sheria ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawaziri katika wizara husika wanatakiwa kusimamia misingi yote inay...