Posts

LORI NOAH ZAUA 5 NA KUERUHI 4 MKOANI KILIMANJARO

Na.Issack Gerald Watu watano Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamepoteza maisha na wengine wanne wakijeruhiwa. Aajali hiyo ambayo imehusisha lori kugongana uso kwa uso na Noah imetokea maeneo ya kikavu kwa Sadala. Daktari wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano. Aidha Dkt.Temba amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai. Kwa upande wa majeruhi Dkt.Temba amesema wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RIPOTI KAMILI YA MAHAKAMA KUU SAKATA LA CUF HII HAPA

Image
MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi juu ya Maombi ya Zuio dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri dogo la madai [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2 kutoka Mahakama Kuu ni kama ifuatavyo; 1.Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. 2.Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF [Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote KUJADILI juu ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. 3.Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF [WAPELEKA MAOMBI -APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI YAO ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO YALIYOWASILISHWA MBELE YAKE. 4.Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliwekwa na Lipumba na ...

WATENDAJI WALIOGAWA MAENEO KWA WANANCHI KIHOLELA KUCHUKULIWA HATUA

Image
Serikali imeziagiza halmashauri nchini kuanza kuchukua hatua kwa watendaji walio husika kugawa maeneo ya makazi kwa wananchi kiholela. Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na Makazi Anjerina Mabula alipokuwa akijibu maswali yaliyo ulizwa na baadhi ya wabunge walio taka kujua kwanini serikali inaadhibu wananchi kwa kubomoa makazi yao na kuwaacha watendaji walio idhinisha. Ameongeza kusema kuwa hatua zinachukuliwa na serikali kuhakikisha hakuna uonevu dhidi ya wananchi. Nisiku ya  tatu tangu mkutano wa tisa wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kwake mjini Dodoma. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMEKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UGANDA

Image
Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Watanzania waishio nchini Uganda katika Mji wa Masaka na kuwahakikishia kuwa hatua zilizoanza kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mabadiliko zimeanza kuzaa matunda. Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mawaziri na viongozi wakuu wa taasisi za Serikali ametaja baadhi ya matokeo hayo kuwa ni kusimamia vizuri uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia 7, kudhibiti mfumuko wa bei hadi asilimia 5.1, kuokoa Shilingi Bilioni 238 walizokuwa wanalipwa watumishi hewa kwa mwaka na kuondoa watumishi wenye vyeti feki waliokuwa wakilipwa Shilingi Bilioni 142 kwa mwaka. Matokeo mengine ni kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi Bilioni 850 hadi wastani wa Shilingi Trilioni 1.2 kupitia Mamlaka ya Mapato ( TRA ), kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ( Standard Gauge ) kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma umbali wa kilometa 726 amba...

MAHAKAMA KUU IMETENGUWA KUFUKUZWA WABUNGE 8 NA MADIWANI 2 WA CUFU

Image
Mahakama Kuu leo imetengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananchi,CUF na kusitisha pia mchakato wa kuwafukuza uanachama mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. Aidha Mahakama hiyo pia imemzuia Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa,Prof.Ibrahim Haruna Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF kujadili kuhusu uanachama wa Wabunge na Madiwani hao. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma ya CUF Taifa, imeeleza kuwa, Mahakama Kuu imekubaliana na Hoja za Wabunge 8 wa chama hicho na imeona hoja za msingi za madai yao zinazopaswa kuangaliwa kuhusu uhalali wa masuala yote yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama hiyo. Imefafanua kwamba, Mahakama Kuu pia imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliyowekwa na Prof. Lipumba na Wenzake katika shauri hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MARAIS MAGUFULI NA MSEVEN WAMETOA MAAGIZO KWA MAWAZIRI WA NCHI ZOTE MBILI

Image
Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni wamewaagiza Mawaziri wa nchi hizi mbili kujadiliana juu ya namna ya kuongeza biashara kati ya nchi hizi ili kupata manufaa makubwa zaidi ya uhusiano na ushirikiano wa kidugu uliopo. Viongozi hao wametoa kauli hiyo leo baada ya kufanya mazungumzo rasmi na kisha kuzungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda ambako Mhe.Rais Magufuli ameendelea na ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku 3. Mhe. Rais Magufuli amesema kwa muda mrefu biashara kati ya Tanzania na Uganda imekuwa ni takribani shilingi Bilioni 200 kwa mwaka kiasi ambacho ni kidogo mno ikilinganishwa na fursa zilizopo, uhusiano na ushirikiano wa kidugu uliojengwa tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere. Kuhusu hatua ambazo Tanzania imeanza kuchukua Mhe.Rais Magufuli amesema pamoja kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango ...