Posts

VIWANDA 100 VIPYA MKOANI KATAVI LINATEKELEZEKA

Na.Issack Gerald-Katavi Mratibu wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoani Katavi Bw.Torokoko Kayumba amesema agizo la kuwa na viwanda vipya 100 kila mkoa katika kipindi cha mwaka mmoja linatekelezeka. Bw.Kayumba ametoa kauli hiyo mapema na kusema wameanza kutekeleza agizo hilo na tayari wana viwanda vipya viwili ambavyo vipo katika hatua ya awali. Amefafanua kuwa kwa sasa serikali Mkoani Katavi   imetenga maeneo katika kila halmashauri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda huku akiwaomba wananchi kujitokeza katika kuanzisha viwanda. Kwa mujibu wa Bw. Torokoko Mkoa wa katavi Kwa sasa una jumla ya viwanda vidogo   329,viwanda vya Kati 3 huku viwanda vikubwa kukiwa hakuna hata kimoja. Kauli hiyo inakuja ikiwa leo ni siku ya uzinduzi kitaifa wa agizo hilo unaofanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na mgeni rasimi ambaye ni waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Suleimani Jafo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

ZIMAMOTO NA UOKOAJI-TAFUTENI VIBALI KABL YA KUJENGA

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi limetoa wito kwa wananchi   kupata vibali vya ujenzi wa nyumba zao ili kupunguza ujenzi holela. Hayo yamebainishwa na kamishina msaidizi jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa katavi Kuhindi ambapo amesema majanga mengi yanatokea kwa kutofuata taratibu za namna bora ya ujenzi wa makazi. Amesema wananchi wanaojenga bila kufuata taratibu na kupata kibali wanasababisha ugumu wa uokoaji katika maeneo hayo pindi majanga mbalimbali yanapotokea. Hata hivyo amesema kupungua kwa gharama kutoka kiasi cha shilingi 150,000 hadi Shilingi 50,000 kumetokana na tathimini ya muda mrefu ambayo ililenga kuondoa vikwazo kwa kundi kubwa la wananchi ambao wasingeweza kumuda gharama hizo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUBAKA MWANAFUNZI

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Mahakama ya wilaya ya  Mpanda  Mkoani Katavi  imemuhukumu kifungo cha maisha Lazaro Ngomalala(50)mkazi wa  Kijiji cha Sibwesa  wilayani Tanganyika baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili(9)wa shule ya msingi Sibwesa. Akisoma hukumu hiyo juzi,hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa alisema mahakama imeridhika na ushahidi wa  mashahidi  sita wa upande wa mashitaka  uliotolewa mahakamani hapo ukiwemo wa mwanafunzi aliyebakwa. Kabla ya kutoa hukumu  hiyo Hakimu  Tengwa  alisema mtu  yoyote  anayefanya kitendo kama alichofanyiwa  mtoto huyo  anakuwa  amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria   namba 130(1)na(2) na kifungu cha  sheria namba 131(3) cha  kanuni ya adhabu. Hakimu Tengwa  alisema ...

ZIARA YA SIKU 3 YA MAGUFULI NCHINI UGANDA

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi umefanyika katika kijiji cha Luzinga, jirani na mpaka wa Mutukula. Pia wamefungua kituo cha forodha chenye huduma zote muhimu kurahisisha safari kati ya nchi hizo mbili. Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000. Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu ya rais nchini inaeleza kuwa rais atakuwa na ziara ya siku tatu nchini humo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI HALMASHAURI YA NSIMBO WALILIA BARABARA

Na.Issack Gerald-Katavi Wakazi wa kata ya Itenka iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali kuwatengezea barabara ya Imilamate-Itenka hadi mjini Mpanda. Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo,wamesema licha ya barabara hiyo kuwa kitovu cha mawasiliano lakini imetelekezwa na serikali. Wamsema wanahofia uhakika wa barabara hiyo kupitika hasa katika musimu huu wa mvua kwani imekuwa ikikatika na wao kubaki wako kisiwani. Akijibu hoja z a wananchi hao,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Raphael Kalinga amesema tayari halmashauri imeshawasilisha makadirio ya barabara zote kwa wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) wanachosubiri ni utekelezaji Bwana Kalinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo bado barabara hiyo ipo kwenye mchakato wa matengenezo. Mwaka 2016 barabara kutoka Kitongoji cha Tumaini-Imilamate-Itenka ilikuwa imewekewa changalawe na hivyo kupitika kwa muda tofauti na hali ilivyokuwa. Kata hiyo ni moja ka...

WAKAZI MKOANI KATAVI WAMETAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME

Na.Issack Gerald-Katavi Wakazi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuwa walinzi wa kutunza miundo mbinu ya umeme ili wapate huduma nzuri na kupunguza kukatika kwa umeme mara kwa mara. Wito huo umetolewa na meneja wa shirika la umeme (TANESCO) mkoani katavi mhandisi Julius Sabu ambapo amesema wananchi wamekuwa wakichangia kuharibika kwa miundombinu hiyo. Ametaja baadhi ya magari marefu kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha kukatika nyaya za umeme na hivyo kusababisha hitilafu na hatimaye usumbufu kwa watumiaji wa nishati hiyo muhimu. Aidha amesema shirika la umeme linafanya utaratibu wa kutenganisha laini za makazi ya watu na maeneo ya viwandani ili kuondosha tatizo la kukatika kwa umeme unaotokana na matatizo yanayosababishwa na viwanda kutumia laini moja na watumiaji wa kawaida. Hata hivyo amewaomba wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa pale wanapoona kuna shida ya umeme katika maeneo yao ili kurahisisha kazi na kutatua changamoto kwa haraka. Habari zaidi ni P5TANZAN...