Posts

EKARI 100 ZATENGWA MKOANI RUKWA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA-Septemba 7,2017

Image
Aliyesimama ni Mh. Bupe Mwakang'ata Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.

FIDIA KWA WANANCHI MKOANI KATAVI-Septemba 7,2017

Image
Mh.Roda Kunchela mbunge viti maalumu Katavi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani NAIBU waziri wa ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano Mh.Edwin Ngonyani amesema kila mwananchi anayesitahili kupewa fidia kutokana na ujenzi wa lami kutoka Mpanda kuelekea Mkoani Kigoma atapewa fidia yake kwa mjibu wa sheria.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KULETEWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-Septemba 7,2017

Image
Mh.Suleiman Kakoso Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini Mh.Suleiman Jafo Naibu waziri(TAMISEMI) SERIKALI imesema imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 700 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi hususani kituo cha afya cha majalila kilichopo makao makuu ya wilaya ya Tanganyika.

NEEMA SEKTA YA AFYA-MKOANI RUKWA-Septemba 7,2017

Image
Naibu waziri Suleiman Jafo NAIBU waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh.Suleiman Jafo amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni   251 kwa ajili ya mkoa wa Rukwa ambapo kati ya kiasi hicho shilingi Bilioni 68 zinatarajiwa kutumika kukamilisha majengo ya vituo mbalimbali vya huduma za afya vilivyopo mkoani Rukwa.

TUMBUA TUMBUA VIGOGO WA SERIKALINI YABISHA HODI TENA-Septemba 7,2017

Image
Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

ZIMAMOTO MKOANI KATAVI NYUMBA KWA NYUMBA KUEPUSHA HATARI-Septemba 6,2017

Image
JESHI la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi limesema linaanza oparesheni ya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba  kubaini watu wenye tabia ya kuchimba vyoo au visima na kuacha bila kufukia  mashimo hayo  hali ambayo husababisha vifo vya watu wanapokuwa wametumbukia katika mashimo hayo.

TAARIFA MPYA KUHUSU UCHAGUZI WA KENYA-Septemba 6,2017

Image
Baada ya kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga kutangaza kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi Mkuu mpaka Tume ya Uchaguzi ifanyiwe mabadiliko, sasa good news kwake ni kwamba, Tume hiyo imetangaza kundi la watu sita ambalo litasimamia uchaguzi huo.