Posts

OFISI ZA WANASHERIA AKIWEMO MTOTO WA RAIS FATUMA KARUME NA LAURENCE MASHA ZATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO-Agosti 26,2017

Image
Sehenu ya majengo ya Ofisi Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo.

MANISPAA YA MPANDA YAPATA HATI SAFI UDHIBITI HESABU ZA SERIKALI,RC APONGEZA-Agosti 26,2017

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Msaafu Raphael Mugoya Muhuga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga  ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Mpanda kwa kupata hati nzuri  ya udhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2016.

HOFU JUU YA EBOLA YATANDA MKOANI RUKWA-Agosti 26,2017

Image
Kirusi cha Ebola WAKAZI mkoani Rukwa wametakiwa kuondoa hofu kutokana na kuwepo kwa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa ebola baada ya mgonjwa mmoja kulazwa na kuendelea kupatiwa matibabu Katika hospital ya mkoa ya Sumbawanga anaeugua ugonjwa wenye dalili kama za homa ya Ebola.

RC RUKWA AZUIA UUZWAJI NJE MADINI YA CLINKER -Agosti 26,2017

Image
Bandari ya Kasanga RC-Rukwa-mbele-ya-Madini-ya-Clinker- Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHALAANI UCHOMAJI MOTO MAKAZI YA WATU KATAVI-Agosti 25,2017

Image
CHAMA cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi kimelaani kitendo cha uchomaji wa makazi ya watu wanaodhaniwa kuwa wanaishi katika hifadhi ya misitu na kuitaka serikali kutafakari upya  suala hilo.

TFS WASISITIZA KUWATIMUA WANANCHI WANAOVAMIA HIFADHI ZA MISITU-Agosti 23.2017

WAKALA wa huduma za misitu nchini TFS  Mkoani Tabora imeendelea kusisitiza azma yake ya kuwaondoa wananchi wote waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi kufuatia uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi hao kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu.

TAMKO LA DED NKASI KUWALINDA WANAFUNZI WENYE UALBINO DHIDI YA JUA KALI-Agosti 23.2017

MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Julius Kaondo amewapiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kuacha tabia ya kuwafanyisha kazi ngumu na kwenye jua kali wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuwa kufanya hivyo wanawahatarisha afya zao na kupelekea kupata saratani ya ngozi.