Posts

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHALAANI UCHOMAJI MOTO MAKAZI YA WATU KATAVI-Agosti 25,2017

Image
CHAMA cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi kimelaani kitendo cha uchomaji wa makazi ya watu wanaodhaniwa kuwa wanaishi katika hifadhi ya misitu na kuitaka serikali kutafakari upya  suala hilo.

TFS WASISITIZA KUWATIMUA WANANCHI WANAOVAMIA HIFADHI ZA MISITU-Agosti 23.2017

WAKALA wa huduma za misitu nchini TFS  Mkoani Tabora imeendelea kusisitiza azma yake ya kuwaondoa wananchi wote waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi kufuatia uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi hao kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu.

TAMKO LA DED NKASI KUWALINDA WANAFUNZI WENYE UALBINO DHIDI YA JUA KALI-Agosti 23.2017

MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Julius Kaondo amewapiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kuacha tabia ya kuwafanyisha kazi ngumu na kwenye jua kali wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuwa kufanya hivyo wanawahatarisha afya zao na kupelekea kupata saratani ya ngozi.

WAZIRI NCHEMBA ATISHIA KUWAFUTIA URAIA WATANZANIA WABAGUZI-Agosti 23.2017

Image
WAZIRI wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba ametishia kuwafutia uraia watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao walikuwa wakimbizi kwa muda mrefu kutokana na tabia ya ya baadhi yakubaguana kitaifa na kikanda. Waziri Mwigulu Nchemba

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA EKARI 2400 KWA AJILI YA UWEKEZAJI,SEKTA YA UFUGAJI,KILIMO,BIASHARA,UTALII,HUDUMA ZA JAMII NA MAKAZI YA WATU KUPEWA KIPAUMBELE-Agosti 21,2017

HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda mkoani katavi imesema  imetenga eneo la Luhafwe lenye ukubwa wa  ekari  2400  kwa ajili ya uwekezaji.

UGOMVI WA MKULIMA NA MFUGAJI WASABABISHA MAJERUHI KATAVI-Agosti 21,2017

WATU wawili wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuzuka ugomvi uliosababishwa na  kile kilichodaiwa ni kupishana kauli kati ya mkulima na mfugaji katika kijiji cha mbugani kata ya Kakese iliyopo manispaa ya Mpanda.

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA FUNGUZI WA MKUTANO WA 37 WA SADC MJINI PRETORIA-Agosti 19,2017

Image
Viongozi wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa  mkutano wa  37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria  ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.