Posts

MADAI YA WAKAZI WA KITONGOJI CHA MGOLOKANI MKOANI KATAVI KUDAI KUWAMIWA NA SERIKALI NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAO WAKATI WA OPARESHENI YA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU KUWAKUTANISHA VIONGOZI WA WILAYA YA MPANDA KUSAKA SULUHU-Agosti 15,2017

Image
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi ijumaa ya wiki hii,inatarajia kukutana na Uongozi wa Wilaya ya Mpanda pamoja na viongozi wa hifadhi ya misitu Wilayani Mpanda, kujadili madai ya wananchi wa kitongoji cha Mgolokani kilichopo kijiji cha Matandalani kata ya Sitalike halmashauri ya Nsimbo wanaodai kuvamiwa na Serikali na kuharibu makazi yao kwa madai yanayotolewa na serikali kuwa wakazi hao wamejenga makazi yao katika eneo la hifadhi ya misitu.

WAZIRI WA AFYA MH.UMMY MWALIMU KUWASILI KESHO MKOANI KATAVI KUZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA-Agosti 15,2017

Image
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu WAZIRI wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu anatarajia kuwasili kesho mkoani Katavi kwa ajili ya kuzindua zoezi la siku  tano la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MKURUGENZI MKUU WA NHIF-Agosti 12,2017

Image
Katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi(by P5 TANZANIA) Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Bw.Benard Hezron Konga kuwa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF.

SERIKALI YA MTAA MKOANI KATAVI YAHOFIA MAFURIKO YA WANAFUNZI-Agosti 12,2017

SERIKALI ya mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,Imeiomba Manispaa ya Mpanda kuandaa miundombinu ya madarasa ya kutosha katika shule ya msingi Nsambwe,ili kukidhi idadi ya wanafunzi itakayoongezeka katika shule hiyo baada ya wakazi wa mtaa wa msasani na tambukareli kuhamia eneo hilo wakiwa na wanafunzi.

RAIS UHURU KENYATTA ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYA-Agosti 12,2017

Image
Uhuru Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.

IEBC YASEMA MFUMO WAKE HAUKUDUKULIWA-Agosti 10,2017

Image
Afisa mkuu tume ya Uchaguzi Kenya Ezra Chiloba Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki.

RTO KATAVI:WAMILIKI IMARISHENI MAGARI YENU KABLA YA SAFARI-Agosti 9,2017

Wamiliki wa magari katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani katavi wametakiwa kuhakikisha magari yao yanakuwa imara kabla ya kuyaigiza barabarani.