Posts

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MKURUGENZI MKUU WA NHIF-Agosti 12,2017

Image
Katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi(by P5 TANZANIA) Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Bw.Benard Hezron Konga kuwa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF.

SERIKALI YA MTAA MKOANI KATAVI YAHOFIA MAFURIKO YA WANAFUNZI-Agosti 12,2017

SERIKALI ya mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,Imeiomba Manispaa ya Mpanda kuandaa miundombinu ya madarasa ya kutosha katika shule ya msingi Nsambwe,ili kukidhi idadi ya wanafunzi itakayoongezeka katika shule hiyo baada ya wakazi wa mtaa wa msasani na tambukareli kuhamia eneo hilo wakiwa na wanafunzi.

RAIS UHURU KENYATTA ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYA-Agosti 12,2017

Image
Uhuru Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.

IEBC YASEMA MFUMO WAKE HAUKUDUKULIWA-Agosti 10,2017

Image
Afisa mkuu tume ya Uchaguzi Kenya Ezra Chiloba Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki.

RTO KATAVI:WAMILIKI IMARISHENI MAGARI YENU KABLA YA SAFARI-Agosti 9,2017

Wamiliki wa magari katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani katavi wametakiwa kuhakikisha magari yao yanakuwa imara kabla ya kuyaigiza barabarani.

RC KATAVI ATAKA WATENDAJI WA VIJIJI KUWA NA DAFTARI LA WAKAZI-Agosti 9,2017

Mkuu wa Mkoa wa katavi meja jenerali mstaafu  Raphael muhuga  amewataka watendaji wote wa vijiji mkoani hapa  kuwa na daftari la wakazi katika maeneo yao.

OPARESHENI BOMOABOMOA YAENDELEA KULIZAWAKAZI MKOANI KATAVI-Agosti 9,2017

WAKAZI wa kitongoji cha Mgolokani Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kurejeshewa ardhi yao au kuwatafutia maeneo ya kuweka familia zao kufuatia kufukuzwa na nyumba zao kubomolewa ambapo serikali imedai kuwa wakazi hao wanaishi ndani ya misitu ya hifadhi.