BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyopo Mkoani Katavi wameunga mkono tamko la Rais linalowataka kufunga mashine zinazotoa risiti za kielekroniks Bw.Malick Saidi ambaye ni Meneja kwa kampuni ya Mafuta ya GBP,kwa upande wake amesema mfumo huo utawaokolea muda pamoja na kampuni yake kukusanya mapato yote kama inavyotakiwa. Aidha Bw.Saidi akatoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi kutokana na mfumo wa mashine za kielektroniks Wiki iliyopita,zaidi ya vituo vya mafuta 700 kote nchini vikiwemo vitano vilivyopo Mkoani Katavi vilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kuikosesha serikali mapato kutokana na kutotumia mashine za kielektroniks EFD. Rais John Magufuli juzi akiwa Mkoani Kagera,ametoa siku 14 kwa makampuni ya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga mashine hizo kinyume na hapo kampuni ambayo haitatekeleza agizo hilo Rais ameagiza ifungiwe na kunyang’anywa leseni ya Biashara. Muuzaji na mnunuzi wote wanajikuta hatiani kwa kukiuka ...