Posts

WAKAZI WA INYONGA WILAYANI MLELE WAENDELEA KULIA NA TATIZO LA UKOSEFU WA UMEME-Julai 11,2017

Image
WAKAZI wa Kata ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwapelekea umeme wa uhakika ili kuchochea maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.

WAKAZI WILAYANI MLELE WATAKA MIFUGO IDHIBITIWE KULINDA MAZINGIRA-Julai 11,2017

WAKAZI wa mtaa wa Katandala kata ya Majimoto Mkoani Katavi,wameuomba uongozi kushughulikia uzururaji holela wa mifugo.

MTOTO MCHANGA AOKOTWA SHAMBA LA MIGOMBA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA- Julai 11-2017.

Image
Rangi ya kijivu ndipo Wilaya ya Kasulu inapopatikana Mkoani Kigoma MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya wiki tatu na Mwezi mmoja wilayani Kasulu mkoani Kigoma ameokotwa katika  migomba  alipotelekezwa na mwanamke asiyejulikana na kutokomea kusiko julikana. Mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Nyakitonto wilayani humo Bw Julius Baligela amesema  mtoto huyo wa njisi ya kike ameokotwa kwenye migomba jirani na mahame ya mtu mmoja akiwa amefungwa kanga. Bw Baligela ameeleza kuwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi wasamalia wema walitoa taarifa wa uongozi na kisha kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya taratibu za kipolisi kukamilika na halamshauri imetoa gari kusafirisha mtoto kuyo kituo cha kulelea watoto Matyazo Kigoma. Aidha Kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji  cha Nyakitonto kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kufanya uchunguzi  kumbaini mwanamke aliyehusika na kitendo hicho. Habarika zaid...

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 56.75 KWA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi (Februari 5,2017 MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mbwana Mhando,amekabidhi hundi ya shilingi milioni 56,750,000 ambayo ni mkopo kwa vikundi 32 vya wajasiliamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando (Mwenye shati nyeupe pichani) akikabidhi mfano wa hundi ya mkpo kwa wajasilimali mbele ya ofisi za kata ya Kabungu.PICHA NA Issack Gerald Februari 5,2017                                              

WAKULIMA CHAMA CHA MSINGI NSIMBO WATAKA WALIPWE PESA YAO

Image
Na.Issack Gerald-Katavi-fEBRUARI 1,2017 WAKULIMA wa zao la Tumbaku wa chama cha Msingi cha Ushirika Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wametaka kulipwa malipo ya mauzo ya tumbaku katika msimu wa kilimo mwaka 2015/2016. Baadhi ya mashamba ya wakulima Nsimbo

WAKAZI KITONGOJI CHA KAMINI HALMASHAURI YA NSIMBO WAOMBA OPARESHENI YA KUWAONDOA KATIKA ENEO LA HIFADHI ISITISHWE.

Na.Issack Gerald-Mpanda-Januari 30,2017 WAKAZI wa kitongoji cha Kamini kilichopo kata ya Ugalla wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamwasilisha barua katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiomba Oparesheni ya kuwaondoa katika kitongoji hicho isitishwe kwa madai kuwa mipaka kati ya kitongoji hicho na misitu ya hifadhi haikufuata taratibu na mipaka kukosewa.

NSIMBO HAINA WATOTO WA MITAANI INA WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI

Na.Issack Gerald-Katavi-Januari 30,2017 Halmashauri ya Wilaya Nsimbo mkoani Katavi imesema kuwa haina watoto ombaomba wa mitaani badala yake ina watoto waishio katika mazingira magumu.