MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 56.75 KWA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi
(Februari 5,2017
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mbwana
Mhando,amekabidhi hundi ya shilingi milioni 56,750,000 ambayo ni mkopo kwa
vikundi 32 vya wajasiliamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando (Mwenye shati nyeupe pichani) akikabidhi mfano wa hundi ya mkpo kwa wajasilimali mbele ya ofisi za kata ya Kabungu.PICHA NA Issack Gerald Februari 5,2017 |
Akikabidhi hundi hiyo katika Ofisi za Kata ya Kabungu kwa
vikundi vya Mshikamano,Muungano na Ibambye kwa
niaba ya vikundi vingine vilivyopo katika Halmashauri hiyo,Mkuu wa Wilaya
ameviagiza vikundi vitakavyokabidhiwa mikopo hiyo kuitumia katika malengo
yaliyokusudiwa.
Mkuu wa Wilaya kabla ya kukabidhi
hundi hiyo,amekagua mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji wa kikundi cha Ibambye
na kushiriki kupalilia karanga za kikundi hicho .
Aidha Mkuu wa Wilaya mbali na
kukabidhi mbegu ya alizeti kwa kikukndi cha Ibambye pia ameahidi kukipatia
kikundi hicho bati 10 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji wa kuku.
Kwa uapnde wake Kaimu Afisa Maendeleo
ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Raymond Fabian Kashindya
amesema,kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri kupitia idara ya maendeleo na
ustawi wa Jamii imetoa mkopo wa Shilingi Milioni 56,750,000 kwa vikundi vya
wajasiliamali katika mwaka huo wa fedha.
Kashindya amesema jumla ya vikundi
ambavyo vimepewa mkopo ni 24 kwa upande wa Wanawake vikiwa na wajasiliamali 119
na vikundi 8 vya vijana vyenye wajasilimali 46 ambapo kwa upande wa wanawake
wamepata shilingi milioni 33,350,000 huku vijana wakipata shilingi milioni
23,400,000.
Kwa upande wao baadhi ya
wajasiliamali waliopokea mkopo huo wamesema,mkopo unatarajiwa kuwanufaisha na
hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo watumishi wa umma wakiwemo
maafisa ugani na ustawi wa jamii wametakiwa kuwaelimisha wananchi katika sehemu
za kazi kuliko kusubiri kufuatwa na wananchi ofisini.
Comments