WAKAZI KITONGOJI CHA KAMINI HALMASHAURI YA NSIMBO WAOMBA OPARESHENI YA KUWAONDOA KATIKA ENEO LA HIFADHI ISITISHWE.
Na.Issack
Gerald-Mpanda-Januari 30,2017
WAKAZI wa kitongoji cha Kamini kilichopo
kata ya Ugalla wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamwasilisha barua katika ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiomba Oparesheni ya
kuwaondoa katika kitongoji hicho isitishwe kwa madai kuwa mipaka kati ya
kitongoji hicho na misitu ya hifadhi haikufuata
taratibu na mipaka kukosewa.
Akizungumza
kwa masikitiko Bw Edward Labati Amala ambaye amewasilisha barua hiyo kwa niaba
ya wananchi wenzake amesema zoezi la kuwaondoa baadhi ya wakazi walio katika
miliki ya hifadhi limefanyika kabla ya kufanyika mkutano wa kijiji uliotarajiwa
kufanyika Januari 29 mwaka huu ukishirikisha viongozi kutoka idara ya misitu
Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Aidha amesema uharibifu wa mali za wananchi ni mkubwa katika Oparesheni hiyo ambapo hata hivyo wananchi hao wameomba wapewe nafasi ya kutunzana kuvuna mazao ambayo yamelimwa na wakazi hao.
Aidha amesema uharibifu wa mali za wananchi ni mkubwa katika Oparesheni hiyo ambapo hata hivyo wananchi hao wameomba wapewe nafasi ya kutunzana kuvuna mazao ambayo yamelimwa na wakazi hao.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Ugalla Mh Halawa Charles Malengeja pamoja na
kusikitishwa na oparesheni hiyo kufanyika kabla ya mkutano wa kijiji kama
ilivyokuwa imepangwa tangu Januari 8 mwaka huu pia amesema hana taarifa rasmi
kutoka Halmashauri juu ya oparesheni hiyo iliyoanza Januari 24.
Hata
hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Mwailwa Smith
Pangani licha ya kusema kuwa atakapopokea barua ya wananchi hao ataipitia na
kuitolea maamuzi pia amesema Oparesheni ya kuwaondoa baadhi ya wananchi
waliovamia maeneo ya hifadhi haitasitishwa.
Aidha Bw
Pangani amesema Oparesheni hiyo iliyoanza Januari 24 mwaka huu itachukua siku
10 ambapo wakati huo huo ametoa wito kwa wakazi hao wanaoondolewa katika eneo
hilo kihamia katika kijiji cha Katambike ambapo kuna maeneo yaliyotengwa kwa
ajili yao.
Januari 8
mwaka huu,Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Mbogo alifany amkutano wa
hadhara katika kitongoji cha Kamini na kupokea kero hizo za wananchi ambapo
ndiye aliyeuagiza uongozi wa kitongoji kwa kushirikiana na wataalamu wa misitu
wafanye mkutano januari 29 kabla ya oparesheni kufanyika tukio ambalo
limekwenda tofauti na ilivyokuwa imepangwa.
Comments