WANAFUNZI WA MAFUNZO YA UFUNDI SHULE YA MSINGI MTAPENDA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WAPOKEA VIFAA VYA UFUNDI
Na.Issack Gerald-Katavi-Januari 30,2017
DARASA linaloendesha shughuli
mbalimbali za ufundi katika Shule ya Msingi Mtapenda Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi,limekabidhiwa vifaa mbalimbali vya ufundi vikiwemo vifaa vya
ujenzi,ufundi seremara na vyerehani
vyenye thamani ya shilingi milioni 1,480,000.
Katika taarifa yake wakati wa
kukabidhi vifaa hivyo katika ukumbi wa Ofisi ya Kata ya Mptapenda,afisa
Mtendaji wa Kata ya Mtapenda Bw.Julius Msilombo pamoja na mambo mengine amesema
kuwa fedha hiyo imetoka katika mfuko wa jimbo jimbo la Nsimbo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya
Mtapenda Mh.Eliezel Fyula ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo
pamoja na mambo mengine amewataka wanafunzi,walimu na waratibu wa kituo hicho
cha ufundishaji kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa ili vitumike kwa sasa na
baadaye.
Aidha Mh.Fyula amewataka wanafunzi
kutumia nafasi ya mafunzo waliyonayo itumike kama njia sahihi ya kujipatia
uzoefu watakaoutumia katika shghuli zao mara baada ya kuhitimu.
Naye Mratibu elimu wa kata ya
Mtapenda Mwalimu Frenk Sankala,akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa
Halmashauri ya Wilaya ya nsimbo mara baada kupokea vifaa hivyo, amesema mahitaji mengine
ambayo yanahitajika ni pamoja na madarasa mawili ya kujifunzia pamoja na mbao
za kutosha kama vifaa vya kujifunzia.
Nao baadhi ya walimu wa Shule ya
Msingi Mtapenda akiwemo mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Geofrey Makundi
mbali na kutoa pongezi kwa waliofanikisha zoezi la upatikanaji wa vifaa
hivyo,wameomba juhudi za kutafuta vifaa vingine zaidi ili kuondokana na tatizo
la kufundisha kwa nadharia.
Wakizungumza mara baadha ya
kukabidhiwa vifaa hivyo,wanafunzi wa mafunzo ya ufundi mtapenda wamesema vifaa
hivyo vitawaongezea ujuzi zaidi wa kujifunza kwa vitendo badala ya nadharia
pekee.
Comments