UZINDUZI SHEREHE ZA MIAKA 40 YA CCM ZAFANYIKA KATUMBA,KITUO CHA AFYA KATUMBA DAWA,MAJI BADO TATIZO



Na.Issack Gerald-Katavi-Januari 30,2017
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kuwa na umoja,ushirikiano na mshikamano ndani ya chama na katika shughuli za maendeleo ya jamii.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Abdallah Muselemo wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM sherehe ambazo zimefanyika Kata ya Katumba.
Awali kabla ya uzinuzi wa sherehe hizo,Diwani wa Kata ya Katumba Mh.Seneta Baraka amesema Kituo cha afya cha Katumba kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama pamoja na umeme wakati huo huo akisema kuwa kuwepo kwa gari la wagonjwa lililotolwa na shirika la wakimbizi duniani UNHCR kumesaidia wagonjwa kwa kiasi kikubwa.
Katika hatua nyingine Mh.Baraka amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto ya miundombinu ya barabara kuwa mibovu,kwa sasa utenenezaji wa barabara yenye urefu wa kilomita 29.8 kutoka geti la Msaginya hadi Kanoge unatarajia kuanza hivi karibuni.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga amekiri kwa kusema kuwa maji yaliyopo Katika kituo cha afya Katumba ni kero kutokana na maji hayo kuwa na kutu na hivyo kutofaa kwa kunywa wala kufulia nguo.
Januari 29,2017

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA