NSIMBO HAINA WATOTO WA MITAANI INA WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI



Na.Issack Gerald-Katavi-Januari 30,2017
Halmashauri ya Wilaya Nsimbo mkoani Katavi imesema kuwa haina watoto ombaomba wa mitaani badala yake ina watoto waishio katika mazingira magumu.

Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo ya jamii kitengo cha Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo Bi Diana Rose Munuo wakati wakati wa mahojiano na mtandao wa P5 TANZANIA Ofisini kwake.
Bi.Munuo pamoja na mambo mengine amesema ongezeko la watoto waishio katika mazingira magumu katika halmashauri hiyo linasababishwa na baadhi ya wanaume kuwazalisha wanawake na kisha kuwatelekeza wanawake waliowazalisha wakiwa na watoto huku huduma za kifamilia zikimtegemea mama pekee ambaye hana uwezo.
Sababu nyingine zinazochangia ongezeko la watoto waishio katika mazingira hatarishi ni mimba za utotoni pamoja na watoto kutelekezwa na wazazi au walezi.
Hata hivyo Halmashauri ina kituo cha Getsman chenye watoto wapato 58 wakiwemo 34 wa kike na 24 wa kiume waishio katika mazingira magumu ambapo wakati huo huo kituo hicho kinahitaji mchango wa wadau ili watoto waishio katika kituo hicho wapate haki zote kama inavyostahili.
Kwa upande wake Bi.Jenifa Fortunate ambaye ni mratibu wa Ukimwi Halmashauri ya Wilaya Nsimbo,pamoja na mambo mengine amesema kuwepo baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu kumetokana watoto kuwa yatima mara baada ya wazazi kufariki kwa Ukimwi.
Aidha,Bi.Fortunate amesema,hivi karibuni Halmashauri ya Wilaya Nsimbo inatarajia kufanya utafiti ili kubaini kwa ujumla hali ya maambukizi ya Ukimwi kwa sasa ambapo Mkoa wa Katavi una asailimia 5.9 ya maambukizi ya Ukimwi.
Katika hatua nyingine Bi.Fortunate ametaja maambukizi ya Ukimwi kuwa moja ya sababu inayochangia kuweko kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi baada ya wazazi au walezi kufariki kutokana na ugonjwa wa ukimwi.
Januari 26 mwaka huu,serikali kupitia kwa Waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa Geoge Simbachawene iliwaagiza wakuu wa mikoa na Wilaya yote hapa nchini kufuatilia kwa kina suala la watoto wa mitaani na kuwachukulia hatua wazazi wanaowatuma watoto wao kuwa ombaomba barabarani katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA