WAKULIMA CHAMA CHA MSINGI NSIMBO WATAKA WALIPWE PESA YAO
Na.Issack
Gerald-Katavi-fEBRUARI 1,2017
WAKULIMA
wa zao la Tumbaku wa chama cha Msingi cha Ushirika Nsimbo Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi,wametaka kulipwa malipo ya mauzo ya tumbaku katika msimu wa
kilimo mwaka 2015/2016.
Baadhi ya mashamba ya wakulima Nsimbo |
Wakizungumza
katika mkutano mkuu wa Mwaka wa chama hicho,wamesema kuwa malipo wanayodai ni
madai ya awamu ya pili ambapo wanadai dola 40 kwa kila kilo iliyozalishwa
katika msimu huo.
Akijibu
hoja hiyo kwa niaba ya Meneja wa Kampuni ya Premium Active Tanzania inayonunua
tumbaku ya wakulima wa chama hicho Bw.Iddy Ramadhani,amesema malipo yanatarajia
kulipwa mwezi Februari mwaka huu ambapo amewataka wakulima kuwa wavumilivu na
mara baada ya fedha kuingizwa katika akaunti ya benki husika zitalipwa kwa
wakulima.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mwailwa Smith Pangani,pamoja na mambo
mengineamewataka wakulima wa chama cha msingi ushirika Nsimbo kulima zao la
kutambaku kwa kuzingatia kanuni za kilimo cha kisasa ili kulima na kupata mazao
yenye ubora na kuwanufaisha.
Aidha
Bw.Pangani amewataka wakulima kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti
wakati wakiendelea na kilimo cha zao la tumbaku.
Katika
hatua nyingine Bw.Pangani amewataka viongozi na bodi ya chama cha ushirika
Msingi Nsimbo kuwa na maadili mema katika uongozi ili iwe mfano kwa
wanaowaongoza ili kuepuka kuwakatisha tama wakulima wa chama hicho na hivyo
kudhorotesha uzalishaji.
Nje
ya Ukumbi Pamoja Radio imezungumza na baadhi ya wanachana ili kutoa maoni ya
semina na mkutano ambao wameufanya.
Katika
hatua nyingine Bw.Mahila Kiula wa Boharia ya chama cha Msingi cha Ushirika
Nsimbo kimetoa taswira na mikakati ya uzalishaji tumbaku kwa mwaka wa fedha
2017/2018 ambapo wamesema wanatarajia kuzalisha kilo milioni 1,250,000 huku
wakitarajia wakulima 1321 kulima zao hilo.
Kabla
ya mkutano wa leo,jana kulifanyika semina kwa wakulima wa chama hicho ambapo
katika mkutano wa leo wakulima zaidi ya 700 kati ya zaidi ya 900 waliotakiwa
kuwepo wamehudhria.
Chama cha Msingi cha Ushirika
Nsimbo kinaundwa na vijiji 14 ambavyo ni Songambele ,Isanjandugu ,Mwenge, Mtakuja,
Uruwila,Mtapenda,Ibindi,Isinde,Ikondamoyo,Kapalala,Matandalani,Kanoge na Mwenge
Barabara
Comments