Posts

SHILINGI MIL.1 YA MKOPO YATOLEWA NA MBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI KWA VIKUNDI 4 VYA WAJASILIAMALI KATA YA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA

Vikundi 4 kati ya 28 vya wajasiliamali vilivyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo vimekabidhiwa mkopo kwa Shilingi milioni Moja kwa ajili kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

WALIMU WAGOMA KUFUNDISHA WAKIPINGA MWALIMU MWENZAO KUPIGWA NA AFISA ELIMU,CWT KUTOA TAMKO LEO

WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.

WANAKIJIJI KASOKOLA MKOANI KATAVI WAKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI,KUSOMWA UPYA MEI 12 MWAKA HUU.

Wananchi wa kijiji cha kasokola kata ya kasokola manispaa ya mpanda wameikataa taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa   katika mkutano wa hadhara ambapo haijasomwa takribani mwaka mmoja na miezi mine.

WIKI YA WAUGUZI MKOANI KATAVI YAZINDULIWA WAGONJWA KUPATIWA MATIBABU BILA MALIPO HADI MEI 12 KILELE CHA MAADHIMISHO

WAUGUZI na Madaktari Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametiwa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kupuuzia maneno na vitendo vya watu wanaowakatisha tamaa ya kufanya kazi za utoaji huduma ya afya kwa ufanisi.

BODI YA CHAMA CHA MSINGI CHA USHIRIKA MPANDA KATI YAVUNJWA

BODI ya chama cha msingi cha ushirika cha wakulima wa tumbaku maarufu kama Mpanda Kati imevunjwa.

JERA MIAKA 7 MPANDA KWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANYANYIFU

MAHAKAMA   ya mwanzo mjini Mpanda imemuhukumu mtu     mmoja kwenda jela miaka saba   kwa kukutwa na hatia ya kujipaia fedha kwa njia ya udanganyifu.

MKUU WA WILAYA YA MPANDA APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima amepokea madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni saba na nusu ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za Wilaya ya Mpanda.