JERA MIAKA 7 MPANDA KWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANYANYIFU
MAHAKAMA ya mwanzo mjini Mpanda imemuhukumu mtu mmoja kwenda jela miaka saba kwa kukutwa na hatia ya kujipaia fedha kwa
njia ya udanganyifu.
Akitoa
hukumu hiyo,hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bw Silivesta Makombe,amemtaja
mtuhumiwa kuwa ni Bw Asubisye
Mangonda (54) mkazi wa Kawajense.
Makombe
amesema,mshtakiwa alijipatian kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kumuuzia
shamba Dominiki Pesambili mkazi wa Kasimba ambalo halikuwa mali yake halali.
Kufuatia
hukumu hiyo,mahakama imetoa onyo kali
kwa watu wenye tabia kama hiyo,kwani
kufanya hivyo ni kinyume na sheria
za nchi .
Mwandishi:Esther Lameck
Mhariri :Issack Gerald
Endelea kufuatilia P5
TANZANIA MEDIA
Comments