MKUU WA WILAYA YA MPANDA APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima
amepokea madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni saba na nusu ili
kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za Wilaya ya Mpanda.
Msaada wa madawati hayo umetolewa leo
na Chama cha msingi cha ushirika Mpanda Katai ambapo msaada huo umekabidhiwa na
Amani Rajabu Ambaye ni Meneja wa Chama hicho.
Akizungumza katika makabidhiano hayo ambayo
yamefanyika katika Ofisi za Chama hicho,Bw.Mwamlima pamoja na shukrani kwa
msaada huo,pia ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano huo.
Katika mgawanyo wa madawati
hayo,Halmashauri ya wilaya ya Mpanda itapata madawati 50 huku Manispaa ya
Mpanda pia ikipata madawati 50.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda ameagiza kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa madawati hayo.
Katika hatua nyingine,amewaagiza
wakurugenzi wa Halmshauri za Wilaya na Manispaa ya Mpanda kuhakikisha hakuna
utoro mashuleni kabla ya kuendesha oparesheni ya kusaka wanafunzi watoto.
Mwandishi:Esther Lameck
Mhariri :Issack Gerald
Endelea kufuatilia P5
TANZANIA MEDIA
Comments