HALMASHAURI KATAVI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI KUSAIDIA KAYA MASKINI BIMA YA AFYA
MKUU
wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral
Mstaafu Raphael Muhuga,amezitaka Halmashauri zote za mkoa wa Katavi kutenga
fungu katika bajeti zake na kuzilipia kaya maskini ili zinufaike na mfuko wa
jamii CHF.
Rai
hiyo ameitoa leo katika uzinduzi wa mfuko huo uliozinduliwa katika kijiji cha Kakese
mbugani Manispaa ya Mpanda mkoani hapa.
Aidha
Muhuga amesema kila mwananchi anatakiwa
kujiunga na mfuko huo ili kupunguza
gharama za matibabu wanapopatwa na maradhi wanapokuwa hawana fedha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa mfuko huo Kitaifa Bw.Eugen Mikongoti,ameupongeza Mkoa
wa Katavi kwa kushika nafasi ya 5 kitaifa kwa uchangiaji wa Mfuko huo wa jamii.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kakese
waliojitokeza katika uzinduzi huo ,wamepongeza hatua ya viongozi wa mfuko wa
bima ya afya kuwafikia katika maeneo hayo kutoa elimu ya faida ya kujiunga na
bima na hasara ya kutojiunga na mfuko huo.
Aidha
Mkurugenzi wa mfuko huo Kitaifa Bw.Eugen Mikongoti,amewataka wakati wa Mkoa wa
Katavi kwa ujumla kutambua kuwa kujiunga katika mfuko ni tahadhari ambayo itamsaidia
kupatiwa matibabu kwa urahisi na gharama ndogo.
Mwandishi:Vumilia
Abel
Mhariri
: Issack Gerald
Endelea kufuatilia P5
TANZANIA MEDIA
Comments