WAKULIMA CHAMA CHA USHIRIKA CHA MSINGI MPANDA KATI WAHAKIKISHIWA MALIPO YA MAUZO YA TUMBAKU ASILIMIA 100.
Na.Issack Gerald-Katavi
Wakulima wa zao la tumbaku wa chama
cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamehakikishiwa
kulipwa asilimia 100 ya uuzaji wa zao hilo, kwa msimu wa mauzo ya 2015/2016.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa
chama hicho Bw.Aman Rajabu wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake kuhusu soko la zao hilo
linalotarajia kuanza hivi karibuni.
Aidha,Bw. Rajabu amewataka wakulima
wa tumbaku kuepuka watu wanaowashawishi kuuza zao hilo nje ya kampuni
iliyosajiliwa ili kuepuka hasara inayoweza kuwapata.
Wakati huo huo,Meneja huyo amewataka
wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha ushirika Mpanda kati kuzingatia sera ya
serikali ya upandaji miti ili kuepuka kuzuiwa kuendesha kilimo hicho kwa sababu
ya kutopanda miti.
Chama cha msingi cha ushirika Mpanda
Kati chenye wanachama wapatao 1600,kilisajiliwa mwaka 2014 na kwa mwaka
2015/2016 Jumla ya miti laki tisa na elfu sitini (960,000) imekwishapandwa na
wanachama hao.
Comments