Posts

PITIA VICHWA VYA MAGAZETI LEO AGOSTI 08,2015 UPATE HABARI KUBWA TANAZANIA NA NJE YA TANZANIA

Image

UVAMIZI OFISI ZA CCM SUMBAWANGA RUKWA,SAMANI ZA MWENYEKITI VYATUPWA NJE

Na.Mwandisi wetu-SUMBAWANGA. Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa chama cha Mapinduzi, juzi wameivamia ofisi ya chama hicho ya wilaya ya Sumbawanga mjini.

IGP MANGU ZIARANI KATAVI KESHO NA KESHO KUTWA

Image
Mkuu wa Jeshi  la polisi Tanzania IGP Ernset Mangu Na.Issack Gerald-Katavi MKUU wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali Ernest Mangu anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Katavi kuanzia tarehe 9 hadi 11 mwezi huu. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Katavi,ASP. Dhahiri Kidavashari, imesema kuwa katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, IGP Ernest Mangu,  atakuwa na fursa ya kuzungumza na wadau mbali mbali katika hoteli ya Lyamba Lya Mfipa majira ya jioni. Katika hafla hiyo waalikwa watapata chakula cha jioni pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi hapa nchini.

UNAMFAHAMU MAGUFULI NA MAISHA YAKE TANGU KUZALIWA HADI SIASA?ONGEZA CHAKULACHA UBONGO NA P5 TANZANIA

Image
Mhandisi John Pombe Magufuli JOHN POMBE MAGUFULI Magufuli ni Nani? Lakini je Daktari John Magufuli ni Nani? Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania. Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera. Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati. Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia. Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT . Alizaliwa Oktoba 1959 Mhandisi John Pombe Magufuli wakati akijiunga na ccm 1995  Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge. Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1...

WAKAZI MPANDA WANDELEA KUWA GIZANI UMEME KUKATIKA,VIWANDA VYAKOSA UMEME SHUGHULI ZASIMAMA KWA MWEZI SASA

NA.Issack Gerald TATIZO la kukatika Umeme mara kwa mara Mkoani Katavi   limesababisha kuzorota kwa biashara ya mchele, kutokana na kukwama kwa ukoboaji wa mpunga zao linalotegemewa na wakazi wengi   mkoani Katavi.

MGOGORO WA ARDHI MTAA WA NSEMULWA BADO MBICHI,MKURUGENZI ATOA JIBU BILA SULUHU

NA.Issack Gerald-Katavi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema haijapokea malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Nsemulwa kutopimiwa viwanja vyao na kutozwa kiwango kikubwa cha pesa tofauti na kilichopangwa kupitia mikutano.

UHAKIKI MAJINA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MANISPAA YA MPANDA WAKWAMA,MKURUGENZI KUTOA TAARIFA BAADA YA VIFAA KUAWASILISHWA

NA.Issack Gerald-KATAVI ZOEZI la uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura limeelezwa kuchelewa kuanza katika Manispaa ya Mpanda kutokana na kucheleweshwa kwa vifaa, zikiwemo mashine za BVR.