Posts

UKAWA WAMPITISHA RASMI LOWASSA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

Image
  Edward Lowassa Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM Chama cha demokrasia na maendeleo chadema   leo kimemuidhinisha Edward lowasa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika   mwezi Oktoba mwaka huu.  Wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema uliofanyika   leo Jijini   Dar Es salaam wamepiga kura ya   kuridhia kiongozi huyo aliyejiunga na upinzani akitokea chama tawala CCM kuwa mgombea   Kiti hicho cha   urais   Kupitia chama hicho.  Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa Nchini amekuwa   akiyagawa   maoni ya Watanzania tangu akihame chama cha Mapinduzi na Kuhamia chama cha   chadema   tang u vikao vya uteuzi vya ccm   kumpitisha mgombea wa urais kulikata jina lake. Hata hivyo katibu mkuu wa chadema Wilbroad Slaa hakuhudhuria mkutano huo mkuu Kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa hakufurahishwa   na uamuzi wa chadema kumpo...

VIONGOZI WA UMMA TANZANIA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KUPITIA WANAOWAONGOZA

  Na.Issack Gerald-KATAVI Viongozi wa umma hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Uzalendokatika kutekeleza mahitaji ya wanaowaongozana siyo kwa maslahi binafsi.

WENYE SIFA YA KUPIGA KURA KATAVI WATAKIWA KUHAKIKI MAJINA YAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

Image
Nembo ya tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania Na.Tume ya taifa ya Uchaguzi-KATAVI WANANCHI   Mkoani Katavi wametakiwa Kufika katika Vituo vyao walivyojiandikishia   Katika daftari la Mpiga Kura ili kuhakiki taarifa zao   Katika daftari la hilo. Kwa Mjibu wa Tangazo lililotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Zoezi hilo limeanza Augost Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandiksha Kuhakiki taarifa zao zilizokosewa kabla ya Muda wa Kupiga Kura. Jaji mstaafu Damian Lubuva mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzio Tanzania Pamoja na Mkoa wa Katavi Mikoa mingine inayotakiwa kuanza zoezi hilo ni Rukwa,Njombe,Iringa,Mtwara,Lindi,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.

JAMII KATAVI,KIGOMA YATAKIWA KUWA NA UTAWALA BORA MATUMIZI YA RASILIMALI

Na.Issack Gerald-Katavi Jamii katika mikoa ya Katavi na Kigoma imetakiwa kutumia sera ya utawala bora kutunza vyanzo vya rasilimali katika mazingira yanayoizunguka kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

BREAKING NEWS

Habari zilizotufikia hivi punde, Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda mkoani katavi Kupitia katibu wa chama hicho Bi Elizabeth Kasmiri ametangaza matoteo ya kura za maoni katika jimbo la uchaguzi la Mpanda mjini ngazi ya Ubunge ambayo ni kama ifuatavyo 1. Sebastian Kapufi 7,190 2. Galos Mgawe 2,359 3.Gabriel Mnyere 2000 Kufuatia matokeo hayo Sebastian Kapufi ametangazwa rasimi kuwa mgombea kiti cha ubunge kupitia Chama cha CCM mpanda mjini. Katika hatua nyingine Jimbo la Mpanda vijijini wakati matokeo yakiendelea kuhesabiwa,matokeo yaliyotangzwa pia na Bi Elizabeth Kasmiri yanayoonesha  kama ifuatavyo 1.Suleimani Kakoso 5,313 2.Wiliam Makufwe 1,872 3.Abdalah Sumry 1,685 Bado zoezi la kuhesabu kura  katika kata tano zilizobaki linaendela,endelea kuwa nasi kwa undani wa uahabri kadri tunavyoendelea kuzipata kutoka katika vyanzo vyetu vya habari.

WATUMISHI WA UMMA MPANDA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA SIASA WAKATI WA KAZI

Image
Watumishi wa umma wakiwa katika Ukumbi wa shule ya Sekondari St.Mary's Mpanda katika semina iliyoendeshwa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo Watumishi mbalimbali katika manispaa ya Mpandaa katika Semian ukumbi wa Shule ya Sekondari St.Mary's Manispaa ya Mpanda katika kikao cha utum,ishi wa umma kikendeshwa Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo Na. Mark Ngumba-MPANDA WATUMISHI Wa Umma wametakiwa Kutojihusisha na Maswala ya Siasa wakati wa Kazi na badala yake wahakikishe wanatimiza wajibu wao wa  Kuwahudumia wananchi Katika Maeneo yao ya Kazi.

JESHI LA POLISI KATAVI LAWATAKA WANANCHI KUWA MAKINI MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BVR

Na.Mark Ngumba-MPANDA JESHI La polisi Mkoani Katavi limewataka wananchi Kuwa Makini na Ujumbe unaosambazwa  Katika Mitandao  ya Simu kwa Madai ya Kuhakiki taarifa za watu waliojiandikisha Kupiga kura Kwa Kutumia mashine za Kimtandao BVR.