JESHI LA POLISI KATAVI LAWATAKA WANANCHI KUWA MAKINI MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BVR
Na.Mark Ngumba-MPANDA
JESHI La polisi Mkoani Katavi
limewataka wananchi Kuwa Makini na Ujumbe unaosambazwa Katika Mitandao ya Simu kwa Madai ya Kuhakiki taarifa za watu
waliojiandikisha Kupiga kura Kwa Kutumia mashine za Kimtandao BVR.
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Kaimu
Mpelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Katavi Inspekta Boke Simango wakati akitoa
Ufafanuzi wa Makosa ya Kimtandao Katika Kikao kilichowakutanisha walimu wote wa
Shule za Msingi Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Aidha Inspekta Simango amewataka
wananchi watakaopokea Ujumbe wa aina hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya Usalama
Wakati huu ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wake.
Comments