OFISI ZA MFUKO WA BIMA YA AFYA NHIF ZAFUNGULIWA KATAVI
Wanachama wa Mfuko wa hifadhi ya afya
ya jamii NHIF Mkoani Katavi wanatarajia
kunufaika na huduma hiyo itakayo kuwa
ikitolewa Mkoani hapa badala ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kama ilivyokuwa awali.
Hayo yameelezwa leo na Meneja wa mfuko
wa taifa wa bima ya afya NHIF Mkoani Katavi Clement Masanja wakati akizungumza
na Mpanda Radio fm.
Aidha Masanja ameongeza kuwa mwanachama halali wa NHIF anapewa nafasi ya
kupata huduma ya Kutibiwa mahali popote Nchini ambapo katika Mkoa wa katavi ofisi
za NHIF zimefunguliwa mwezi june mwaka huu kwa lengo la kusogeza huduma kwa
wanachama wake.
Comments