WATUMISHI WA UMMA MPANDA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA SIASA WAKATI WA KAZI
Watumishi wa umma wakiwa katika Ukumbi wa shule ya Sekondari St.Mary's Mpanda katika semina iliyoendeshwa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo |
Na. Mark Ngumba-MPANDA
WATUMISHI Wa Umma wametakiwa
Kutojihusisha na Maswala ya Siasa wakati wa Kazi na badala yake wahakikishe
wanatimiza wajibu wao wa Kuwahudumia
wananchi Katika Maeneo yao ya Kazi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Vicent Kayombo Katika
Mkutano uliowakutanisha walimu wote wa shule za Msingi Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda wenye lengo la Kupanga Mikakati
ya Kuimarisha Kiwango cha Ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2015.
Mkutano huo wenye lengo la
kutathimini utendaji wa kazi za Idara ya
Walimu kwa kipindi cha Miezi sita iliyopita Umewashirikisha Jumla ya walimu 500
kutoka shule zote za Msingi Katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Comments