WENYE SIFA YA KUPIGA KURA KATAVI WATAKIWA KUHAKIKI MAJINA YAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA
Nembo ya tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania Na.Tume ya taifa ya Uchaguzi-KATAVI WANANCHI Mkoani Katavi wametakiwa Kufika katika Vituo vyao walivyojiandikishia Katika daftari la Mpiga Kura ili kuhakiki taarifa zao Katika daftari la hilo. Kwa Mjibu wa Tangazo lililotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Zoezi hilo limeanza Augost Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandiksha Kuhakiki taarifa zao zilizokosewa kabla ya Muda wa Kupiga Kura. Jaji mstaafu Damian Lubuva mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzio Tanzania Pamoja na Mkoa wa Katavi Mikoa mingine inayotakiwa kuanza zoezi hilo ni Rukwa,Njombe,Iringa,Mtwara,Lindi,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.