JARIBIO LA KUUA KWA IMANI ZA USHIRIKINA WATU SITA WASHIKILIWA
Na.Issack Gerald-Katavi
Watu
sita wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kutaka
kuvamia na kufanya mauaji ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi.
Kamanda
wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuwa limetokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Ikola kata ya Ikola tarafa ya Karema Wilayani Mpanda.
Kidavashari
amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi kituo cha Ikola
limefanikiwa kuzima jaribio hilo la mauaji na kuchoma moto kituo cha polisi kwa
tuhuma za kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Mpalamawe B kukataa kutajwa kwa
wanadhaniwa kuwa wachawi hadharani.
Aidha
ametoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa
taarifa katika vyombo vya usalama.
Comments