ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 ZA MADAI YA WALIMU MKOANI KATAVI HAWAJANUSA
Chama Cha walimu Tanzania CWT
Mkoani Katavi kimesema madai mbalimbali ambayo walimu wanaidai serikali mpaka
sasa hayajalipwa.
Hatua hiyo imethibitishwa na
Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi Hamis Ismail Chinahova wakati akizungumzia kuhusu
hatua iliyofikiwa ya kulipwa kwa madeni ya walimu.
Aidha amesema kiasi cha cha
shilingi bilioni 1.3 ambacho walimu Mkoani Katavi wanaidai serikali kinahusu
madai ya likizo,uhamisho,matibabu,masomo na stahiki nyingine muhimu ukiondoa
suala la mishahara.
Kwa mjibu wa taarifa ya
iliyokuwa imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango hivi
karibuni,takwimu ya madeni ya watumishi nchini inaonesha ni zaidi ya
shilingi bilioni 127 kati ya hizo walimu wakidai shilingi bilioni 16.25
zilizotakiwa kulipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments