RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA WAWEKEZAJI MABILIONEA WA UJERUMANI NA DENIMARK


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli amesema siku za hivi karibuni anatarajia kukutana na Wakurugenzi Watendaji wawili kutoka nchi za Ujerumani na Demark watakaokuja kufanya uwekezaji nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo Machi 19,2018 wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara,ambao ulikuwa umebeba maudhui ya ‘Tanzania ya Viwanda na Ushiriki wa sekta binafsi nchini.’
Rais Magufuli amesema watakuja kufanya uwekezaji wa kiwanda kipya cha Petroli Kemikali (Petrol Chemical Plant) ambacho kitakuwa na thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.92 ambayo ni sawa na takriban Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.56.
Ameeleza kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4000 katika eneo la Kilwa kwa ajili ya kutengeneza mbolea ambayo itauzwa ndani pamoja na nje ya nchi kwa kutumia gesi iliyopo nchini.
Wakati huo huo,amewataka wawekezaji waliopo hapa nchini kutumia fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini kwa kuwa rasilimali zipo za kutosha huku akiwataka watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Kwa upande wao wafanyabiasahara na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwaslisha changamoto zinazowakwamisha katika suala uwekezaji ambapo miongoni mwa kero zinagusa masuala ya nishati ya umeme, madini, bandari, kodi, ushuru, usafiri, kilimo na biashara.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA