JAJI MKUU WA TANZANIA ATOA WARAKA MZITO KWA MAHAKAMA MKOANI KATAVI
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Khamisi Juma ametoa waraka kwa Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa
wa Katavi unaokataza Tozo ya malipo kwa hati za hukumu ambazo
ilikuwa inatozwa kwa wananchi .
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Khamisi Juma |
Kwa mjibu wa Afisa mawasiliano
na Tehama wa mahakama hiyo Jemes Vedasi Kapele amesema waraka huo unaelekeza
usitishwaji wa tozo za hati za hukumu.
Aidha Afisa huyo amesema kufutwa kwa tozo hizo kutakuwa
mkombozi kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini kwani walikuwa wakishindwa
kumudu gharama zinazotakiwa kutokana na ukosefu wa fedha wanapohitaji kuapitwa
haki zao kwa mjibu wa sheria.
Mara kadhaa baadhi ya wananchi
wamekuwa wakionekana kutumia baadhi ya aseti kama ardhi ili kugharimia gharama
zinazohitajika.
Jaji mkuu ametoa waraka huo
ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kufanya ziara mkoani Katavi na kutoa
kauli ya kufuta tozo hizo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments