WAKAZI MJINI MPANDA:KUKATIKA UMEME KERO-Oktoba 4,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Baadhi ya Wakazi mjini mpanda Mkoani
Katavi wakiwemo wafanyabiasha wameliomba
shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Katavi Kuboresha miundombinu yao ili
kukomesha tatizo la kukatika umeme mara kwa mara mjini hapa.
Baadhi ya wakazi hao wakiwemo Prisca Joseph na Wambura
Mabula wamesema umeme ndio nyenzo kubwa ya kuendesha shughuli zao hivyo
kukatika kwake kunaathiri hali ya kipato kwa kila mmoja.
Katika taarifa yake aliyoitoa hivi
karibuni Afisa uhusiano wa Shirika hilo
mkoani Katavi bwana Amoni Michel Bidebuye
amekiri kuwepo changamoto hiyo na kuahidi kuendelea kuzitatua kwa nguvu
zote.
Licha ya TANESCO mkoani katavi
kuboresha mitambo yao ya kuzalisha umeme, shirika hilo bado halijaweza
kufanikiwa kutoa umeme wa uhakika kwa wateja wake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments