EQUIP TANZANIA WATOA SHILINGI BILIONI 6 KWA AJILI YA ELIMU KATAVI NA SINDIDA-Oktoba 4,2017
Na.Issack Gerald-Katavi
RC Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhaiano ya mpango huo |
Haatua hiyo imebainishwa na Bonifasi
Joseph ambaye ni Ofisa mkuu wa usimamizi wa fedha EQUIP Tanzania,Katika Mkutano
wa kuzindua Mpango huo katika Mkoa wa katavi uliofanyika jana katika manispaa ya Mpanda na kusema kuwa
fedha hizo hupelekwa moja kwa moja katika halmashauri husika.
Amesema Mpango huo unafanya kazi na
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI ambapo fedha hizo
zinazoletwa Tanzania ni fedha za ruzuku na sio Mkopo.
Mgeni Rasmi Katika Uzinduzi wa Mpango
huo Mkoani Katavi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneal Mstaafu Raphael
Muhuga amezielekeza halmashauri zote kusimamia fedha hizo kwa umakini na
pasijitokeze uzembe au ubadhirifu wa
aina yoyote sambamba na kutoa taarifa kwa wakati na zenye usahihi.
Wakati huo huo Mpango huo utawapatia
pikipiki waratibu elimu kata,
kuwafundisha walimu wakuu na walimu wakuu wasaidizi namna ya kutayarisha
mipango ya maendeleo ya shule ikiwa pamoja na kupatiwa vishikwambi (Simu kubwa
Tableti) ili kuboresha usahihi wa taarifa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Mpanda Bi Lilian Charles Matinga amewataka waratibu elimu katika Halmashauri za
Nsimbo na Manispaa ya Mpanda zilizo chini yake kuzisimamia fedha hizo ili
zitumike kama zinavyotakiwa.
Mratibu Kiongozi wa Mradi wa EQUIP
Tanzania Mkoani Katavi amesema Mkoa wa katavi licha ya kufanya vizuri katika
elimu ya Msingi Lakini bado kuna baadhi ya changamoto ambazo anaamini mradi huu
unazitatua na kuboresha zaidi kiwango
cha elimu Mkoani Katavi
Kwa upande wake Afisa elimu Mkoani Katavi
Mwl. Ernest Hinju amesema Kupitia Mradi huu utasaidia kumaliza baadhi ya
chanamoto mbalimbali kama kuanzisha shule shikizi katika maeneo ambayo
hayana shule,Pamoja na kumalizia ujenzi wa madarasa ambayo hayajakamilika.
EQUIP Tanzania Kiutekelezaji Nchini
Tanzania umeanza rasmi Mwaka 2014 katika mikoa mitano ya Tabora,Kigoma,
Shinyanga,Dodoma pamoja na mkoa wa simiyu na baada ya matokeo mazuri ya
utekelezaji wa Mpango huo ikaongezwa Mikoa miwili ambayo ni Lindi na Mara na
ulitegemewa kumalizika Mwezi januari mwakani lakini tathmini iliyofanyika kumekua na matokeo mazuri sana ya mpango huo
na hivyo kujitokeza fursa ya kuongeza miaka mingine miwili mpango ambao
umekwenda samabamba na kuongeza mikoa
mingine miwili ya Katavi na Singida.
Steven Myamba ni kiongozi wa Mpango
huo ambaye amepewa jukumu la kusimamia mpango katika mikoa mine ikiwemo ya Katavi
na Tabora ili kuhakikisha malengo yanakusudiwa.
Mwandishi:Mdaki Hussein,Mhariri
:Issack Gerald
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments