DC MPANDA KUSHUGHULIKIA VIBOKO WAVUNJA NDOA ZA WATU NA KUHARIBU MAZAO SHAMBANI-Oktoba 4,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
MKUU wa wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga
amesema atawasiliana na idara ya maliasili pamoja na Shirika la kuhifadhi mbuga
za wanyama Tanapa Mkoani Katavi ili kushughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu
tatizo la viboko wanaotishia maisha ya binadamu na kuharibu mazao shambani kwa
wakazi wa kijiji cha milala na maeneo jirani.
Matinga ametoa kauli hiyo leo ambapo amesema pamoja na mambo mengine Ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata iandike barua
kuelezea tatizo lililopo ili lishghulikiwe haraka iwezekanavyo.
Wiki iliyopita
wakazi wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo,mitaa ya Kigamboni na
Makanyagio, waliilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko ambao
wanaharibu mazao shambani pamoja na kusababisha baadhi ya ndoa kuvunjika
kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao shambani ili kukabiliana na wanayama
hao huku viongozi wa kijiji kupitia kwa afisa mtendaji wa kijiji cha milala
Bw.Antipas Kalumbete akisema mara kwa mara wamekuwa wakiandika barua za kuomba
msaada lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Bwawa la
milala ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa
Manispaa ya Mpanda, linasemekana kwa sasa lina viboko zaidi ya tehelathini
wanaoharibu mazao shambani na kusababisha wakazi wa maeneo jirani na bwawa hilo
kulazimika kujifungia ndani majira ya jioni wakiogopa kushambuliwa.
Katika
Mkoa wa Katavi kumekuwa na wanyama pori wakiwemo pia simba kuvamia makazi ya
watu na kuleta madhara kwa binadamu ambapo kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu amesema kuna ulazima wa hatua kuchukuliwa
ni wakazi wake Katika Manispaa ya Mpanda waendelee kuwa salama huku akisem
tatizo la viboko limekuwa likijitokeza mara kwa mara.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
Ukurasa P5Tanzania Limited
Comments