DC MPANDA:SITAMBUI KAMA WANANCHI WANAISHI CHINI YA MITI-Oktoba 4,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wakiwa chini ya mwembe kama makazi yao baada ya makazi yao kubomolewa(PICHA NA Issack Gerald) |
Matinga ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mwafaka wa uhalali wa waliokuwa wakazi wa
kitongoji cha Mgolokani wanaodai kuvamiwa na serikali katika makazi yao na
kuondolewa kimakosa pamoja na kuharibiwa mali zao.
Aidha matinga amesema kama
Halmashauri iliidhinisha wakazi hao kujenga makazi katika kitongoji cha
Mgolokani kinachodaiwa kuwa sehemu yam situ wa msaginya ilifanya kosa inatakiwa
iwajibike katika tatizo hilo.
Hivi karibuni mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Raphael Kalinga alisema suala hili linashughulikiwa
na vyombo vya kisheria ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la
Nsimbo Mh.Richard Mbogo takribani wiki moja iliyopita aliwataka wananchi kuendelea
kuwa wavumilivu wakati wakisubili kurejeshewa maeneo yao mara baada ya vyombo
husika kuchukua maamzi.
Wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wanadai kuishi katika kitongoji hicho kuanzia mwaka 1974 ambapo mwezi Julai mwaka huu 2017 wahifadhi wa misitu walifika kuhakiki mipaka na wakazi hao kuhakikishiwa kuwa wao wako eneo salama hali ambayo iliwaacha na mshangao nyumba zao zilipoanza kubomolewa.
Wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wanadai kuishi katika kitongoji hicho kuanzia mwaka 1974 ambapo mwezi Julai mwaka huu 2017 wahifadhi wa misitu walifika kuhakiki mipaka na wakazi hao kuhakikishiwa kuwa wao wako eneo salama hali ambayo iliwaacha na mshangao nyumba zao zilipoanza kubomolewa.
Zaidi ya kaya 200 zilibomolewa makazi
yao kwa madai kuwa walivamia msitu wa hifadhi wa Msaginya na kujenga makazi
pamoja na kuendesha shughuhuli za kibinadamu suala ambalo linakanushwa na
wananchi hao.
Maeneo mengine yaliyokumbwa na
oparesheni ya watu kuondolewa katika makazi yanayodaiwa kuwa sehemu ya hifadhi
ya misitu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni kaya ya Litapunga na
Kitongoji cha Makutanio.
Comments