Posts

Showing posts from 2017

RAIS MAGUFULI,KENYATTA,NKURUNZIZA,IDRISI,MAHAKAMA YA KENYA NA JSEHI LA ZIMBABWE WATUNUKIWA TUZO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii. Rais Magufuli mwenye miwani katika picha Marais wengine ambao wamepata tuzo ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye amejishindia tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya. Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao. Rais wa Taasisi ya Mandela,Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi ...

WATUMISHI WA HOSPITALI MKOANI KATAVI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA YUMO MWANANCHI ALIYESAHWISHI KUTOA SHILINGI 500

Image
Na.Issack Gerald-Katavi TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa ( Takukuru) Mkoani Katavi imewafikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Katavi watuhumiwa watatu  wakiwemo  watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa. Kwa Mjibu wa taarifa ya Mkuu wa Takukuru Mkoani Katavi John Minyenya kwa vyombo vya habari,amewataja wauguzi wa Hospitali hiyo waliofikishwa mahakamani kuwa ni Yohana Paul Deo(25) mkazi wa Kawajense anayetuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 40,000 kutoka kwa mwananchi aliyekuwa akimuuguza mgonjwa wake baada ya kupata ajali ya pikipiki na kuvunjika mguu na mkono. Deo katika kesi hii,anadaiwa kuomba fedha hiyo Septemba 22 mwaka huu ili amsaidie ndugu wa mgonjwa huyo kupatiwa huduma baada ya kukaa siku mbili hospitalini hapo bila kuhudumiwa. Muuguzi mwingine ambaye amefikishwa mahakamani ni Marco Bunduki James(31) mkazi wa Kawajense ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shi...

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LAAMUA KUJITATHMIN

Image
Jeshi la Polisi Zanzibar,limeamua kujitathmini kwa lengo la kusahihisha kasoro watakazobaini ili kutoa huduma bora kwa jamii. Mpango huo wa kujitathmini unafanyika kwa utaratibu wa kusikiliza maoni na ushauri kutoka kwa wananchi,wakilenga zaidi kujenga imani ya raia kwa jeshi hilo. Utaratibu huo wa kujitathmini ulitangazwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis Ahmed kuwa wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuliweka jeshi karibu na jamii na kufanya kazi pamoja ya kupambana na vitendo uhalifu. Huu ni utaratibu mzuri wa kufanya mawasiliano na raia ambao unafaa kuendelezwa kwa maeneo yote ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo imeelezwa kuwa utaratibu huu utaondoa au kupunguza kwa kiasi kikubwa uadui au hofu iliyojengeka kati ya raia na polisi. Aidha ni nafasi nzuri kwa maofisa wa Jeshi la Polisi kuwaelimisha raia na kuwaeleza dosari wanazoziona katika jamii katika kupambana na vitendo vya uhaifu na kuwatia hatiani wanaofanya vitendo hivyo. Chanzo:Zanzibar...

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUZIMWA KWA 'CHANELI' ZA BURE KWENYE VING'AMUZI

Image
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema, kwa mujibu wa sheria iliyopo sasa vituo vyote vya runinga ambavyo vimepewa leseni ya FTA (Free to Air) vinapaswa kuonekana hata baada ya kifurushi kwenye kisimbusi kwisha. Dkt.Hassan Abbas Ufafanuzi huu unatolewa kufuatia uwepo wa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa huduma ya runinga za bure pindi vifurushi katika visimbusi (ving’amuzi) vyao vinapomalizika Dkt.Abbas amesema hadi sasa kuna vituo 16 vya runinga vya ndani ya nchi vilivyopewa leseni hizo vikiwemo vituo vya ITV,Clouds TV na Channel 10. Amesema ili mtumiaji atazame Runinga hata baada ya kufurushi chake cha malipo kwisha,kituo cha runinga (mfano ITV) kinapaswa kuwalipa warushaji wa masafa (mfano Azam) ili ITV iweze kuonekana kwa wananchi hata ambao hawajalipia visimbusi vyao. Wakati huo huo Dkt.Abbas ametahadharisha kuwa, endapo kituo cha runinga hakitawalipa wasafirishaji wa masafa watakatiwa huduma na hivyo kuwafanya wananchi washindw...

MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO WATAALAMU WA MAKOMBORA KOREA KASKAZINI

Image
Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea Kaskazini akidai wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol Wizara ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na kusema kuwa wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya masafa marefu wa Korea Kaskazini. Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu huku Korea Kaskazini ikisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita. Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini Marekani na hata kutwaliwa kwa mali yao zilizo nchini Marekani. Wanaume hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora. Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo Korea Kaskazini i nasema y...

KWA MWAKA 2017 WAPO WENGI WALIOTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI,HAWA NI BAADHI YA VIGOGO

Image
Katika mwaka 2017, mambo mengi yametokea ambayo yametikisa nchi kuanzia kwenye nyanja ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Imekuwepo mijadala mikubwa sana kuanzia kwenye ajali za barabarani, uchumi wa nchi, utawala, na mambo mengine yanayogusa maisha ya wananchi. Rais Dkt John Magufuli Wakati zikiwa zimesalia siku 6 mwaka 2017 kuisha, na mjadala sasa ukiwa ni sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya na suala la Wachagga kurudi makwao, tutakuwa hatujautendea haki kama, japo kwa ufupi hatutakumbushana masuala yaliyotokea kwenye siasa kwa mwaka huu. Mwaka huu, neno “Kutumbua” lilishika kasi sana. Hii ni kutokana na Rais Magufuli ambaye alisema amejipa kazi ya kutumbua majipu, kuwafuta kazi viongozi ambao kwake yeye aliona hawaendani na kasi yake au kutokana na sababu nyingine yoyote. Idadi ya waliotumbuliwa ni wengi, na katika mjadala wetu wa leo, tutaangazia vigogo 12 waliotumbuliwa tangu Januari 1, 2017. 1.  Mhandisi Felchesmi Mramba. Januari Mosi 2017, R...

SERIKALI KUANZA KUWASHGHULIKIA WANAOVAA NUSU UCHI

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania. Waziri Harison Mwakyembe Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika. Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED