ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI RUKWA : HAKUNA MWANASIASA ATAKAYERUHUSIWA KUVURUGA AMANI
Na.Issack Gerald Bathromo- Rukwa
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inalinda amani ya nchi kwa
gharama zozote na kamwe haitoruhusu mwanasiasa yeyote kusababisha vurugu
zitakazochochea uvunjifu wa amani.
Waziri Mkuu akiwa Viwanja vya sabasaba Wilayani Nkasi Rukwa(PICHA NA.Issack Gerald) Agosti 23,2016 |
“Hatuzuii
kuwa na vyama vya siasa ila haturuhusu vurugu kupitia vyama vya siasa na hakuna
jambo lisilokuwa na mipaka. Mambo ya kuhamasishana kufanya vurugu
hatutayaruhusu, tunataka watu wafanye kazi,” alisisitiza.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na viongozi wa dini pamoja
na wazee wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kuwasili mkoani humokwa ziara ya kikazi
ya siku mbili.
Alisema
Serikali inataka Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za
kuwaingizia kipato na kuwaletea tija, hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu
kwani vurugu zikitokea hawatakuwa na mahali pa kukimbilia na hakuna shughuli ya
maendeleo itakayofanyika.
“Suala
la uhamasishaji wananchi juu ya utunzaji wa amani ni la lazima hivyo viongozi
wa dini na wazee kwa pamoja tushirikiane katika kukemea vitendo vya uchochezi
kwasababu vurugu zikitokea Watanzania hatuna mahali pa kukimbilia,” alisema.
Aidha,
Waziri Mkuu aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa pamoja na
viongozi wake kwa sababu kazi ya uongozi ni ngumu na inachangamoto nyingi.Pia
aliwaagiza viongozi wa dini wa mkoa wa Rukwa kuharakisha uundwaji wa Kamati ya
Amani ya mkoa huo.
Awali,
Sheikh wa mkoa wa Rukwa, Sheikh Rashid Akilimali amesema madhehebu ya dini
hayawezi kuvuruga amani ya nchi ila anahofu na viongozi wa vyama vya siasa
kutokana na vitendo vyao vya kuhamasisha vurugu.
Kufuatia
hali hiyo Sheikh Akilimali aliwaomba wanasiasa nchini kutovuruga amani kwani
machafuko yakitokea watashindwa kufanya ibada mbalimbali ikiwemo kufunga mwezi
Mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh
Akilimali alisema kwa sasa wananchi wako huru kwenda kufanya ibada misikiti na
makanisani kutokana na uwepo wa amani, hivyo aliwasisitiza wanasiasa kutothubutu
kuichezea amani.
Tafadhalini
wanasiasa msituharibie amani ya nchi yetu. Amani haichezewi tunaona kwa wenzetu
wanavyohangaika, wanaishi kwa tabu sisi hatujazoea kukimbia. Sisi
Watanzania ni moja na tunaishi kwenye nyumba moja hivyo hatuna budi
kushirikiana kuilinda amani yetu,” alisema.
Kwa
upande Katibu wa Wazee mkoani Rukwa, Kanali Mstaafu, John Mzurikwao alimuomba
kiongozi huyo kuwasaidia kutatua kero mbalimbali zinazoukabili mkoa huo
zikiwemo za malipo ya pembejeo kwa mawakala wa kilimo pamoja na mgogoro wa
ardhi katika shamba ya Efatha.
Waziri
Mkuu alisema suala la malipo kwa mawakala wa pembejeo za kilimo linafanyiwa
kazi na watalipwa baada ya Serikali kukamisha zoezi la uhakiki wa madeni hayo
ili kujiridhisha kama kweli wakulima wapatiwa pembejeo na kwa kiwango gani.
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments