WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MKOANI MWANZA WAOMBA KUJENGEWA SEKONDARI YA KATA.
Na.Albert
Kavano-Mwanza.
Wakazi
wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wameiiomba serikali
kuwajengea shule ya sekondari ya kata kutokana na wanafunzi kutembea umbali
wa zaidi kilometa 10 kutafuta elimu kata jirani ya Sangabuye.
Mandari Jiji la Mwanza |
Hayo
yamebainishwa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Iseni
katani humo agenda kuu ya mkutano ikiwa kujadili maendeleo ya mtaa huo ikiwemo
suala la elimu.
Bi
Mariamu Daudi na Bw Josephati Lazaro wamesema watoto wao wanakumbwa na
athari nyingi kutokana na kukosa shule maeneo ya karibu ikiwemo wanafunzi
wakike kubeba ujauzito kutokana na ulaghai wa wapanda pikipiki (
bodaboda).
Aidha
diwani wa kata hiyo Bw James Katoro amesema kuwa lipo eneo la Chasubi
lilotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo lakini kamati na
uongozi wa serikali iliyopita waliuza eneo hilo kinyemela na amewataka
walionunua eneo hilo kusitisha ujenzi mara moja.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments