WAZIRI MKUU WILAYANI SUMBAWANGA : WATUMISHI WATAKAOKULA FEDHA ZA CHF WAFUKUZWE KAZI NA NA WAFIKISHWE MAHAKAMANI
Na.Issack Gerald Bathromo-Sumbawanga Rukwa
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani kwa
watumishi wote wa sekta ya afya watakaobainika kula fedha zinazochangwa na
wananchi kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Pia
amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Zelothe Stephen pamoja na Mganga Mkuu wa mkoa
huo, Dk. John Gurisha kusimamia na kulinda fedha za CHF zinazochangwa na
wananchi na kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye jimbo la
Kwela, Tarafa ya Mtowisa wilayani Sumbawanga.
"Kitendo
cha kula fedha zinazochangwa na wananchi kwa lengo la kupata huduma za afya
kinawafanya wakatetamaa ya kuendelea kuchangia mfuko huo. Kama wako watumishi
wenye tabia hizo waache mara moja," amesisitiza.
Mbali
na kutoa agizo hilo kwa uongozi wa mkoa wa Rukwa, pia Waziri Mkuu amewataka
wananchi kujiunga na CHF kwa sababu mfuko huo utawawezesha kupata huduma
za matibabu bure wao na familia zao katika kipindi cha mwaka mzima.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu
amesema barabara ya kutoka Ntendo hadi Muze ye urefu wa kilometa 85
itajengwa kwa kiwango cha lami ili iweze kupitika kwa urahisi na
kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati.
“Mimi
nilidhani mlima wa Kitonga ndio mkali kuliko yote na eneo la Sekenke ndio
linatisha zaidi!. Kumbe barabara ya kuja huku Mtowisa ndiyo inatisha zaidi
kuliko zote. Lazima tuweke lami ili iendelee kupitika kwa urahisi zaidi,”
amesema.
Akizungumzia
ombi lililotolewa na mbunge wa jimbo la Kwela, Ignas Malocha la kutaka tarafa
hiyo ya Mtowisa kuwa wilaya au halmashauri, Waziri Mkuu amesema analichukua na
kwenda kulifanyia tathmini na majibu atayapata kupitia uongozi wa mkoa.
Malocha
alisema jimbo la Kwela linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
miundombinu ya barabara hali inayosababisha wananchi kushindwa kusafirisha
mazao yao kwa urahisi.
Pia
aliomba ukanda huo wa bonde la mto Rukwa upandishwe hadhi na kuwa wilaya au
halmashauri ili kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Rukwa,
Mhandisi Masuka Mkina ameelezea mkakati wa kuboresha miundombinu ya barabara
mkoani hapa ikiwemo ya kutoka Ntendo hadi Muze wilayani iliyopo wilayani Sumbawanga.
Mhandisi
Mkina amesema Serikali imetenga jumla ya sh. milioni 170 kwa ajili ya kuweka
zege kwa ajili ya kurahisisha upandaji wa mlima hasa kwenye eneo la Kizungu
katika barabara ya kutoka Ntendo hadi Muze.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments