WAZIRI MKUU WILAYANI NKASI : ATAKAYEVAMIA MSITU FAINI MIL. 70, JELA MIAKA SABA
Na.Issack Gerald Bathromo-Nkasi Rukwa
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kuvunja sheria
kwa kuvamia na kuharibu mazingira ya msitu wa Mfili ambao ndiyo chanzo pekee
cha maji cha Wilayani Nkasi atatozwa faini ya sh. milioni 70 pamoja na kifungo
miaka saba jela.
Katika
kuhakikisha hatua zinachukuliwa Waziri Mkuu amemkabidhi mkuu wa wilaya ya
Nkasi, Said Mtanda kitabu cha sheria kitachomuongoza katika kuwachukulia hatua
wale wote watakaobainika kufanya uharibifu katika chanzo hicho cha
maji.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na wananchi wa mji Mdogo
wa Namanyere katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanya vya Sabasaba.
“Mkuu
wa wilaya akishindwa kuwachukulia hatua za kuwaondoa wananchi na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu na
kuanzisha makazi au kufanya shughuli za kijamii naye atakuwa jipu,” alisema.
Waziri
Mkuu alisisitiza kuwa maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa maji baada ya wananchi kuvamia katika vyanzo vya maji na kufanya
shughuli za kibinadamu hivyo kusababisha vyanzo vingi kukakuka
“Serikali
haitakubali kuona mtu anaharibu chanzo cha maji. Wananchi mnatakiwa kuwa
walinzi wa maeneo hayo na atakayekutwa anachunga mifugo, analima, kukata nyasi
au kufanya shughuli zozote za kijamii ndani ya maeneo hayo atachukuliwa hatua
kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Awali
Waziri Mkuu alikagua mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili ambalo mwanzo
lilikuwa na ujazo wa lita 1,500 ambapo litakapokamilika litakuwa na ujazo wa
lija 248,067 hivyo kuwezesha wakazi 82,689 kunufaika.
Akizungumza
kwenye eneo la mradi mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili, Mkurugenzi Mtendaji wa
wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo alisema hadi kukamilika mradi huo unatarajiwa
kugharimu sh trilioni 1.011 ambapo Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa sh.
milioni 500 na OOfisi ya Rais TAMISEMI itatoa sh. milioni 500.
Mkurugenzi
huyo alisema mradi unakabiliwa na changamoto ya ukosefu umeme ppamoja na
mitambo ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme, ambapo aliiomba Serikali
kuipatia halmashauri hiyo sh. milioni 222.576 ikiwa ni gharama za kupeleka
umeme kwenye eneo la mradi na kununua mitambo.
Mbali
na kutembelea mradi wa upanuzi wa bwawa, pia Waziri Mkuu alitembelea hospitali
teule ya wilaya ya Nkasi na kuzindua wodi mpya yenye uwezo wa kulaza wagonjwa
72 kwa wakati mmoja.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments