YA WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KAVUU MKOANI KATAVI ISIKUPITE HII HAPA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Rukwa
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kavuu linalojengwa
na kampuni ya Nandra Engineering and Construction Ltd ya mkoani Morogoro na
kumtaka mkandarasi huyo kulikamilisha haraka.
Daraja la Mto Kavuu linalojengwa(Na.Issack Gerald) |
Ujenzi wa
mradi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 85.34 ulianza Septemba 2013 na
ulitarajiwa kukamilika Septemba 27, 2014.Mradi huo wenye thamani ya sh. Bilioni 2.718 unagharamiwa na Serikali kwa
asilimia 100.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Majimoto, Halmashauri ya
Mpimbwe wilayani Mlele.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kujiepusha na
matapeli wanaopita katika maeneo yao na kuwataka wachange fedha za kuanzisha
vikundi ili wapewe sh. milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali.
Awali
mbunge wa jimbo la Kavuu, Dk. Pudensiana Kikwembe alimuomba Waziri Mkuu kutoa
kipaumbele kwenye ujenzi wa daraja la Kavuu ili likamilike mapema na kuwawezesha
wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Pia
ameiomba Serikali kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ya ujenzi wa
barabara ya kutoka Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilomita 130 kwa
kiwango cha lami aliyoitoa wakati wa kampeni. Waziri Mkuu amesema barabara hiyo
itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Katavi,
Mhandisi Abdon Maregesi akizungumzia maendeleo ya mradi wa ujenzi wa daraja la
Kavuu amesema umekamilika kwa asilimia 50 na unategemea kukamilika Novemba 30
mwaka huu.
Amesema
utekelezaji wa mradi huo umekuwa na kasi ndogo kwa sababu ya uhaba wa fedha,
ambapo tangu mwaka ulipoanza hakuna fedha zilizotolewa kwa miaka miwili
mfululizo (2013/14 na 2014/15) licha ya kuwekwa kwenye bajeti.
Mhandisi
huyo amesema hadi kufikia Agosti 22, 2016 tayari mkandarasi amekwishalipwa
jumla ya sh. bilioni 1.284 ikijumuisha na malipo ya awali. Malipo hayo ni sawa
na asilimia 47 ya mkataba
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments