TATIZO LA MAJI SUMBAWANGA RUKWA KUWA HISTORIA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Rukwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Manispaa ya
Sumbawanga mkoani Rukwa inatarajiwa kupata huduma ya maji safi na salama
kuanzia mwezi ujao baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliokuwa
unajengwa.
Mradi
huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira,
Manispaa ya Sumbawanga (SUWASA), kwa ufadhili wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na
Serikali ya Ujerumani kupitia benki yake ya Maendeleo (KfW), sh. bilioni 31
utakapokamilika.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa
maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga na kuitaka
kampuni ya kampuni ya Techno Fab Gammon Joint Venture ya India kumaliza ujenzi
wa mradi huo haraka iwezekanavyo.
Alisema
mradi huo ambao tayari umekamilika kwa asilimia 85 unatarajiwa kukamilika
Septemba mwaka huu, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na
Manispaa katika kulinda miundombinu ya mradi huo mara utakapokamilika pamoja na
kutunza vyanzo vya maji.
Alisema
kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya vyanzo vya maji ambapo wananchi
wanajishughulisha na shughuli za ulimaji, uchungaji wa mifugo, ujenzi wa nyumba
za makazi na uchomaji misitu hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira na
hatimaye vyanzo hivyo hukauka.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wote wa wilaya na wenyeviti wa vijiji
nchini kuyasimamia maeneo yenye vyanzo vya maji na kuwaondoa watu
wotewalioyavamia kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
Naye
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye
alimuwakilisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge katika
hafla hiyo alisema aliishukuru Serikali ya Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya
kwa kufadhili mradi huo.
Hata
hivyo Mhandisi Kamwelwe alisema suala la kuhifadhi mazingira ni msingi endelevu
wa upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo aliwaomba wananchi kujiepusha na
uchafuzi wa vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira ili kuepuka athari ya
Taifa kukubwa na janga la ukame.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments